Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

ATAKA BUNGE MAALUMU LA KATIBA LIVUNJWE...

$
0
0
Mwenyekiti Samuel Sitta akisisitiza jambo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ameshauriwa kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kuomba kuvunjwa kwa bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma endapo wajumbe wake watashindwa kuanza kujadili rasimu Jumatatu ijayo.

Katika hatua nyingine, Sitta ameshauriwa kusitisha posho za wajumbe wa Bunge hilo ili waanze kushiriki mijadala bure kwa vile hawawatendei haki wananchi kwa kuendekeza malumbano na mabishano yasiyo na tija kwa wananchi.
Mjumbe Michael Lekule Laizer, ambaye ni Mbunge wa Longido, alisema ndani ya Bunge hilo katika mjadala wa  juzi jioni kuwa Mwenyekiti Sitta anapaswa kuandika barua kwa Rais Kikwete kumuomba alivunje Bunge hilo.
“Mheshimiwa Mwenyekiti Bunge hili limeshindwa kazi, kinachoendelea humu ndani ni kuzomeana na kushangiliana kwa mambo yasiyo na msingi.
Kama itafika Jumatatu hatujaanza kujadili rasimu kutokana na mabishano haya, nashauri uandike barua kwa Rais ili alivunje Bunge hili badala ya kuendelea kupoteza fedha za wananchi,” alisema.
Kwa upande mwingine, Mjumbe Constantine Akitanda akichangia katika mjadala huo, alimuomba Sitta kusitisha posho za wajumbe hao ili wajadili bure kutokana na kuendekeza malumbano huku fedha za Watanzania zikiteketea.
“Mheshimiwa Mwenyekiti mimi inaniuma sana, huu utaratibu tunaokwenda nao si mzuri na unawaumiza wananchi wengi.
Kama tutaendelea na malumbano haya basi nakuomba usitishe posho ili tujadili bure, vinginevyo natamani hata kuondoka ndani ya Bunge hili,” alisema Akitanda ambaye baada ya kumaliza kuzungumza alibeba begi lake na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge.
Wabunge hao walitoa maoni yao wakati Bunge hilo Maalum la Katiba, likijadili mabadiliko yaliyofanywa kwenye Kanuni za 37 na 38 za Bunge hilo, yanayotaka kutumika kwa aina zote mbili za kura yaani kura ya wazi na siri katika ufikiaji wa uamuzi  wakati wa upitishaji wa rasimu za Katiba mpya.
Marekebisho hayo ya Kanuni yaliwasilishwa bungeni hapo jioni juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge, Pandu Ameir Kificho  na kuibua mgongano wa hoja baina ya wajumbe wa Bunge hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles