![]() |
Gary Ralston akiwa kwenye chumba alicholala na mwalimu wake huyo (picha ndogo kushoto) usiku mzima. |
Bernadette Smith, mwenye umri wa miaka 35, alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16, Gary Ralston baada ya kumfundisha kwenye shule ya Bannockburn High mjini Stirling.
Baada ya kuponyoka kwenye tundu la sindano kuhukumiwa kifungo jela kutokana na mahusiano hayo, Smith sasa amepigwa marufuku kabisa kufundisha tena.
Smith, ambaye alifanya kazi kama mwalimu wa Historia na Kiingereza kabla ya kusimamishwa kwake, ameelezea mahusiano hayo kama 'siku kumi za wazimu'.
Mahakama ya Stirling ilielezwa mwezi uliopita jinsi mahusiano hayo ya kimapenzi, ambayo yalianza kwa kubusiana kwenye bustani na kuishia kwa yeye kulala usiku mzima kwenye kitanda cha mwanafunzi huyo, kumemgharimu heshima yake.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba Smith aliwaeleza polisi na wenzake alikuwa katika 'mapenzi' na Gary, ambaye aliwahi kumfundisha na kumfundisha twisheni baada ya shule.
Mahusiano hayo yalianza katika darasa la Smith, ambako aliweka bayana hisia zake kwa mvulana huyo, kabla wawili hao kwenda bustanini na kubusiana kwa mara ya kwanza.
Hatahivyo, bibi yake Gary aligundua walichokuwa wakifanya wawili hao na kuitaarifu shule hiyo, ambayo ilimsimamisha Smith mara moja.
Smith, mama wa watoto watatu kisha akatembelea nyumbani ambako Gary alichangia na baba yake, Richard, na yeye na Gary wakakaa usiku mzima pamoja kwenye kitanda cha kijana huyo.
Kisha baadaye akawaeleza polisi kwamba alimweleza Ralston kuhusu hisia zake kwa kijana wake.
Smith alipatikana na hatia ya kujiingiza katika vitendo vya ngono na mwanafunzi wakati akiwa kwenye dhamana ya kuaminiwa kati ya Septemba 13 na 20 mwaka jana.
Aliwekwa chini ya uangalizi kwa miaka miwili kama sehemu ya hukumu ya jamii, ambayo pia ilimweka kwenye daftari la wahalifu wa ngono kwa kipindi kama hicho.
Machapisho yaliyotolewa na Baraza Kuu la Walimu (GTC) jana yamefichua kwamba Smith sasa amefungiwa kabisa kuingia darasani.