Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

MAKABURI KUHAMISHWA KINYEREZI KUPISHA UJENZI WA BOMBA LA GESI...

$
0
0
Makaburi 47 yaliyopo katika eneo la Kanisa Katoliki Parokia ya Kinyerezi, Khanga jijini Dar es Salaam yatahamishwa kupisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mnazi Bay, Mtwara na Songosongo.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala imewataka ndugu na jamaa wa marehemu waliozikwa kwenye eneo hilo kufika ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kinyerezi kujiandikisha ndani ya siku 30 kuanzia jana wakiwa na barua za utambulisho kutoka kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa wanakoishi.
Ujenzi wa bomba hilo la gesi unafanywa na Kampuni ya China Petroleum Technology Development Corporation (CPTDC), ikisaidiana na kampuni za China Petroleum Pipeline Bureau (CPP) na China Petroleum Pipeline Engineering Corporation (CPEC).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles