Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

AFUNGWA JELA MAISHA KWA KUMNAJISI MTOTO MDOMONI...

$
0
0
Mkazi wa  mtaa wa Nsemulwa, Athuman  Mussa (54) amehukumiwa  kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, baada ya kutiwa  hatiani kwa kosa la kumnajisi mtoto  wa kike  mwenye umri wa miaka minne mdomoni.

Hukumu hiyo  ilitolewa  juzi  na Hakimu  Mkazi Mfawidhi  wa mahakama hiyo, Chiganga  Ntegwa  baada ya  kuridhishwa  na ushahidi uliotolewa  mahakamani  hapo  na upande wa mashitaka  uliongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi  wa Polisi, Ally Mbwijo.
Kwa mujibu wa  hati  ya mashtaka, mshtakiwa  anadaiwa  kutenda kosa hilo Juni 26  mwaka jana saa 12:00 jioni  nyumbani  kwake katika mtaa wa Nsemulwa  katika Mji wa Mpanda.
Akisoma hukumu  hiyo, Hakimu  Ntengwa alieleza kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo ambaye  wazazi  wake ni jirani zake  akiwa  anacheza  na watoto wenzake  karibu na nyumba yake akamwita  na kuingia naye ndani  akiahidi kumpatia zawadi  ya  pipi aina ya jojo.
Baada ya mtoto  huyo  kuingia ndani  ya nyumba,  Athumani  alimvuta kwenye kochi  sebuleni na  kisha alimwingizia uume wake  kwenye mdomo wa mtoto huyo  hadi hapo alipomaliza haja yake kisha akamwamuru  aondoke nyumbani kwake  ndipo mtoto  huyo alipotoka mbio  na kurejea kwao  akilia.
Aliiambia mahakama baada ya mtoto huyo kufika nyumbani kwao mama yake alimuuliza  kilichomfanya alie  ndipo  alitema  mbegu za kiume ambazo zilikuwa  mdomoni mwake  na kisha alimwelezea mama yake  kila kitu alichotendewa na  mshitakiwa.
Baada ya mama kuelezwa unyama  huo aliofanyiwa  mtoto wake, naye alianza  kulia kwa nguvu  na kusababisha  majirani kufika nyumbani hapo  ambapo  walielezwa  alichofanyiwa mtoto huyo  ndipo majirani walikwenda nyumbani kwa mshitakiwa  wakamkamata   na kumfikisha kwenye kituo cha polisi.
Ntengwa  alieleza  mahakamani hapo kuwa  mahakama baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi  kwa pande zote mbili  za mashitaka na utetezi, mahakama imemwona mshitakiwa  amepatikana na hatia hivyo kabla ya mahakama haijamwadhibu  ilimpatia nafasi ya mshitakiwa  kusema jambo au kama ana sababu za msingi aombe kupunguziwa adhabu.
Mshitakiwa aliiomba mahakama   imwachie huru kwani  hakufanya kitendo hicho  na  zile  mbegu   za kiume alizotema mtoto huyo  zilikuwa  ni  karanga alizokuwa  akila mtoto huyo.
Mwendesha mashitaka, Mbwijo alipinga utetezi huo  na kuiomba mahakama  itoe adhabu kali kwa mshitakiwa  ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles