![]() |
Jaji Francis Mutungi. |
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amewasihi viongozi wa madhehebu ya dini, wananchi na viongozi wa vyama vya siasa kujitokeza kwa wingi leo kuiombea amani Arusha.
Mutungi alilazimika kurudia mwito huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema Arusha awali iligubikwa na siasa zilizoleta taswira kuwa hakuna amani kutokana na vurugu lakini hivi sasa tofauti hizo hazina budi kumalizika ili wananchi wapate maendeleo na kupata fursa za uwekezaji.
Aliongeza kuwa ofisi yake imeamua kuitisha mkutano huo leo katika Uwanja wa Shekhe Amri Abeid na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, wa vyama na wafuasi wao.
“Amani ya Arusha imevurugwa na masuala ya siasa hivyo mjumuiko wa leo ni kwa ajili ya kuombea amani ili wananchi wafanye shughuli zao kama kawaida, pia uchumi ukue na naomba viongozi wa siasa na dini kuhubiri amani, amani, amani na pia vyama vya siasa vifanye siasa za amani na si chuki,’’ alisema.
Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya Chadema kususia mkutano huo, alisema hoja za Chadema si za kubeza na kuishauri kama inataka aisaidie basi imwandikie barua.
Chadema imekasirishwa na taarifa za Polisi juzi kuhusu ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini kuchomwa moto na wao wenyewe huku Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akidai hawatashiriki mkutano huo kwa sababu hawamtambui Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo ambaye pamoja na mambo mengine ndiye aliyesababisha machafuko na watu kufa.
Mapema jana Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa aliwambia waandishi wa habari akisisitiza kuwa chama hicho hakitashiriki mkutano huo wa amani kutokana na upotoshwaji wa kauli uliofanywa na Ramadhani Kalamba kupita mitaani na kutangaza kwa wananchi kuwa chama hicho (kesho) kimekubali kuafikiana na CCM kwa ajili ya kumtambua Meya wa Jiji hilo, Lyimo.

Kutoka Kahama Mwandishi Raymond Mihayo anaripoti kuwa Chadema imetaka Watanzania hususani wanachama wake kuacha ushabiki wa kisiasa kwa wakati huu mgumu ambao kimo kwenye malumbano na mtikisiko mkubwa kisiasa.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Willibrod Slaa, wakati akihutubia wakazi wa hapa na kuongeza kuwa lengo la chama chake ni kutengeneza misingi ya maisha na kutendea haki Watanzania.
Dk Slaa alisema kuna baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifanya ushabiki wa kisiasa usio na tija hasa kwa wakati mzito kwa chama hicho, kutokana na uchochezi unaofanywa na vyama vya siasa ambavyo hata hivyo hakuvitaja.
Pia alisema Chadema imejipanga vema kukabiliana na vyama vya siasa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kusisitiza kuwa kikubwa zaidi ni kuhusu Katiba ya chama hicho.
“Katiba ya Chadema haikutungwa kumkandamiza Mtei (Edwin-muasisi wa Chadema), Mbowe (Freeman-Mwenyekiti) au Dk Slaa, bali ilitungwa kwa ajili ya kulinda chama na maslahi ya wananchi kwa ujumla,” alisema Dk Slaa.
Akizungumzia mpasuko ndani ya chama hicho, baada ya kuwavua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kabwe Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, Dk Slaa alisema uamuzi huo ulitolewa na chama kwa kufuata misingi ya Katiba na kuongeza kuwa Katiba haiangalii mtu wala cheo.
Pia alisema Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi alipanga kukutanisha vyama vya siasa nchini na kukaa meza moja katika Uwanja wa Shekhe Amri Abeid Arusha, kwa lengo la kuvipatanisha vifanye kazi pamoja.
Pia Msajili alitaka vyama vya siasa viache ubinafsi na badala yake vifanye kazi pamoja kwa kufuata itikadi za vyama vyao hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko baadaye.
Katibu Mkuu yuko katika ziara ya wiki moja katika wilaya za Kibondo, Kakonko, Kasulu, Kigoma Kaskazini, Kigoma Kusini, Kigoma Ujiji katika Manispaa ya Kigoma na wilaya za Tabora, Urambo, Bukene, Nzega, Igunga na Mkoa wa Singida.