Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

MUHIMBILI YAKANUSHA KUWA NA WADI MAALUMU YA BODABODA...

$
0
0
Hospitali ya Muhimbili.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo (MOI), imekanusha uvumi kwamba madaktari wake wamekuwa wakikata miguu madereva wanaoendesha pikipiki za kukodisha maarufu bodaboda, wanapojeruhiwa katika ajali.
Aidha imesikitishwa na uvumi kwamba wametenga wadi maalum kwa ajili ya wagonjwa wa ajali za pikipiki kwa kuwa taarifa hizo si za kweli.
Meneja Uhusiano wa Moi, Jumaa Almasi, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo.
“Taarifa hizo zote siyo za kweli na sisi Moi tunaheshimu  maadili na miiko ya kazi yetu. Jukumu letu ni kuokoa maisha na wagonjwa wote wanatibiwa chini ya mwavuli mmoja bila kujali chanzo cha magonjwa yao,” alisema.
Alisema pamoja na mambo mengine, uamuzi wa kuondoa kiungo chochote cha mgonjwa si jambo rahisi kama inavyodhaniwa,  kwa kuwa lazima mgonjwa mwenyewe atoe ridhaa yake, asaini kukubaliana na uamuzi huo kama anajitambua na kama hajitambui, ndugu wa mgonjwa watahusishwa.
Alisema ikiwa makundi yote hayo hayakupatikana, busara za madaktari na maprofesa zitatumika baada ya tatizo la mgonjwa kujadiliwa kwenye kikao maalum cha madaktari.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles