Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

MSICHANA ALIYEUZA BIKRA YAKE PAUNI 485,000, SASA AAMUA KUINADI UPYA...

$
0
0
Catarina Migliorini.
Mwanafunzi mmoja nchini Brazil ambaye aliuza bikra yake kwa Pauni za Uingereza 485,000 bado anaendelea kuinadi tena kwenye mnada mtandaoni, akidai mapatano ya awali hayakuwahi kukamilika.

Catarina Migliorini, miaka 21, anauza 'ubikira' yake kwa wanunuzi kwa kiasi cha kuanzia Pauni 62,000, lakini anasema anatumaini kuuza walau kwa Pauni 930,000 (sawa na Dola na Marekani milioni 1.5).
'Mnada wa ubikira' wa Catarina awali ulioneshwa kwenye filamu ya Australia, lakini alidai alitapeliwa na mtengenezaji filamu Justin Sisely, na kwamba hakuwahi kupewa pesa hizo ambazo mteja kutoka Japan alilipa kwa ajili yake Oktoba mwaka jana.
Mnada huo ulimfanya Catarina maarufu nchini Brazil na akawa mpenda starehe kwenye nchi yake asilia na Argentina.
"Baada ya kuwa nimeandikwa na vyombo vingi vya habari kwenye nchi nyingi sana, niliamua kwa hakika kuuza bikra yangu," anaelezea kuhusu uamuzi wake wa kuuza tena ubikira wake.
Awali Catarina alisema alitaka kutoa asilimia 90 ya bei ya mauzo ya mnada wa mwisho kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga makazi ya kisasa nyumbani kwake jimbo la kusini la Santa Catarina.
Hatahivyo, wakati akidai kutowahi kupokea pesa hizo - wala kupoteza ubikira wake - mashirika hayo bado hayajapokea msaada wake.
Oktoba mwaka jana, Natsu, miaka 53, milionea wa Japan aliwapiku wazabuni kutoka Marekani Jack Miller na Jack Right, na kimwaga wa India Rudra Chatterjee, kuweza kutembea na mwanafunzi huyo wa elimu ya viungo - ambaye alisema angetumia fedha hizo kujenga makazi kwa mafukara - familia zilizoathiriwa.
Mnada huo ulikuwa sehemu ya filamu hiyo ya Australia iliyobatizwa jina la "Virgins Wanted",  ambayo Sisely angeperuzi maisha ya Catarina na Alex Stepanov, mwanaume ambaye alinadi ubikira wake kwa Dola za Marekani 3,000.
Lakini pale Catarina alipokwenda kukutana na mzabuni wake aliyeshinda, Natsu, kwenye mgahawa mmoja ulioko Sydney, anadai kwamba hakuweza kufikia vigezo ambavyo Sisely alimpatia, na kusisistiza wawili hao hawakufanya mapenzi.
Pia anadai Sisely hakumfidia gharama zake za usafiri, ama kumpatia Pauni hizo 485,000 zilizolipwa na Natsu; na sasa anaamini kwamba 'Natsu' ni kiinimacho tu, na kwamba mnada huo ulikuwa ni mpango wa kuipatia nafasi filamu hiyo kwenye vyombo vya habari.
"Nilikubali kufanya mnada huo, sababu Justin alisema itakuwa njia bora kabisa kuweza kuvivutia vyombo vya habari kuhusiana na mradi huo," alisema.
Sisely, ambaye kwanza alitangaza filamu hiyo mnamo Mei, 2010 na kusema ingehitimishwa kwa mabikira wote hao kufanya mapenzi, amekanusha madai hayo.
"Tunazo picha hizo kuweza kuthibitisha vinginevyo," alifafanua Sisely.
Katika mpango wa kukwepa sheria za ukahaba, Catarina alitakiwa 'kukabidhiwa; kwa mnunuzi wake ndani ya ndege kati ya Australia na Marekani - akihojiwa kabla na baada ya tendo la ngono.
Tendo la ngono lenyewe lisingerekodiwa, alisema Sisely, na Natsu wangemiliki haki ya kutotajwa, bila picha yake kuoneshwa katika vyombo vya habari.
Madai yote ya ubikira wa Catarina na wakati huu yamekuwa yakishughulikiwa kwa mashaka na wataalamu wa tiba huku kukiwa hakuna uthibitisho wa njia yoyote ya kueleza kama mwanamke ni bikira.
Catarina alisaini mradi huo miaka mitatu iliyopita wakati alipoona tangazo lililotolewa na kampuni ya Thomas Williams Productions ikisaka bikira kwa ajili ya kutengeneza filamu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles