Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

BABU SEYA, PAPII KOCHA KUSOTA JELA AMA KUACHIWA LEO...

$
0
0
Papii Kocha na Babu Seya wakiwapungia jamaa zao nje ya Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.
Hatma ya mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ itajulikana leo katika Mahakama ya Rufani Kanda ya  Dar es Salaam.

Mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi  wa kama wanamuziki hao wataendelea kutumikia kifungo cha maisha jela au kuwaachia huru baada ya kupitia upya hukumu iliyowatia hatiani.
Babu Seya na Papii Kocha wanaendelea kutumikia kifungo hicho, baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto katika hukumu iliyotolewa Februari 2010.
Juni 25, 2004 Babu Seya, Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walihukumiwa kifungo cha maisha jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikana na hatia hiyo.
Katika hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanawe kwa makosa 23 ya kunajisi na kulawiti na hivyo kuwapa adhabu ya kifungo hicho.
Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na wanawe walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ambapo Jaji Thomas Mihayo (mstaafu), aliwatia hatiani tena na kuunga mkono hukumu ya Mahakama ya Kisutu.
Hata hivyo, Babu Seya na wanawe hawakuridhika na uamuzi huo na kwenda  Mahakama ya Rufani, ambako hukumu ilibadilika kidogo kwa Mbangu na Francis kuachiwa huru, huku Babu Seya na Papii Kocha wakibaki na hatia na kuendelea kutumikia kifungo hicho.
Kwa mujibu wa hukumu, Mahakama iliridhika na ushahidi ulio kwenye kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo kwa kila kosa na kuwaona Babu Seya na Papii Kocha, wahusika wa kutenda makosa yanayowakabili.
Katika hukumu hiyo utetezi wa washitakiwa kuwa hawakuwa katika eneo la tukio ulikataliwa. Katika hukumu hiyo, Babu Seya alitiwa hatiani kwa makosa matano ya kunajisi na Papii Kocha mawili.
Hivi karibuni, wakiwasilisha hoja zao mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro, wakili wa Babu Seya na Papii Kocha, Mabere Marando aliomba Mahakama iwafutie adhabu hiyo wateja wake, kwa madai kuwa ushahidi uliowatia hatiani, ulikosewa.
Alidai kuwa katika hukumu iliyowatia hatiani, Mahakama Kuu ilikubaliana nao kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilikosea kuchukua ushahidi, lakini walisema haina tija kwa sababu kuna ushahidi mwingine wa kuunga mkono.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles