Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

SIKU 10 ZA MGAWO WA UMEME ZAPUNGUZWA NA KUFIKIA TANO...

$
0
0
Miundombinu ya umeme.
Makali ya mgawo wa umeme yameanza kupungua baada ya asilimia 80 ya gesi kutoka kisima cha Songosongo, kuanza kuzalisha umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, alisema matengenezo katika kisima cha gesi yamefikia asilimia 85 na asilimia 80 ya gesi imeanza kusafirishwa hadi Dar es Salaam kuzalisha umeme.
"Kama mnavyojua, visima vya gesi hatumiliki sisi, wenye mamlaka nayo walikuwa wakifanya matengenezo jambo lililosababisha uzalishaji wa nishati hiyo kwa kutumia gesi kupungua na kuathiri mikoa iliyo kwenye Gridi ya Taifa.
"Tanesco na Serikali tumekuwa tukifuatilia jambo hili kila siku na sasa nimehakikishiwa kuwa kazi hiyo iliyokuwa ikifanyika usiku na mchana, imekamilikwa kwa asilimia 85, hivyo asilimia 80 ya gesi ya kuzalisha umeme itaanza kusafirishwa hadi Dar es Salaam leo (jana) jioni.
"Walitwambia matengenezo yangechukua wastani wa siku 10, lakini tunashukuru wenzetu kwa kuwa ndani ya siku tano wamefanya kazi kubwa ambayo itatoa unafuu wa upatikanaji umeme," alisema Mramba
Alisema Tanesco haikuwa na njia mbadala ya kupunguza tatizo la umeme kwa wateja wake, kwa kuwa kwa sasa umeme mwingi unaotumika unatokana na gesi.
"Hata sisi hatupendi watu wateseke kwa kukosa umeme, ila hatukuwa na njia mbadala ya kukabiliana na tatizo hilo. Mradi wa gesi asilia utakapokamilika nadhani tutaondoa tatizo la umeme nchini," alisema.
Wateja katika mikoa inayopata umeme kutoka Gridi ya Taifa, walianza kupata adha ya upungufu wa umeme kwa siku 11 kuanzia Ijumaa iliyopita na hali hiyo ilitarajiwa kwisha Novemba 26.
Hali hiyo ilitokana na kampuni ya Pan African Energy Tanzania Limited (PAT) kufanyia matengenezo visima vyake vya gesi.
Kutokana na matengenezo hayo, kumekuwa na upungufu wa gesi kutoka kisiwa cha Songosongo kilicho katika wilaya ya Kilwa, Lindi ambayo imekuwa ikizalisha wastani wa megawati 330.
Mikoa na maeneo yaliyokuwa na adha hiyo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida, Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Tabora, Shinyanga, Manyara na Zanzibar.
Akizungumza hali ya mabwawa ya kuzalisha umeme, Mramba alisema tangu mwanzo wa mwaka huu haikuwa nzuri sana kutokana na kuwa na kiasi kidogo cha maji.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles