![]() |
Raila Odinga. |
Hatimaye Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga amekata rufani katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo akipinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika karibuni.
Uhuru Kenyatta alitangazwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika Machi 4, mwaka huu kwa ushindi mwembamba wa asilimia 50.07.
Katika rufani yake Odinga anawashutumu watendaji wa tume hiyo ya uchaguzi kwa kuhujumu matokeo.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu ulioiingiza nchi hiyo kwenye mapigano wa mwaka 2007, ambapo watu zaidi ya 1,200 walipoteza maisha.
Pamoja na kushinda katika uchaguzi huo, Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa kudaiwa kuchochea vurugu hizo.
Baada ya ushindi, Kenyatta alitaja ushindi wake kwenye uchaguzi huo kama ushindi kwa demokrasia na amani. Kenyatta alisema wapiga kura walizingatia sheria na kuahidi kushirikiana na wapinzani wake.
Hata hivyo, Odinga aliahidi kupinga ushindi wa Kenyatta mahakamani akisema kwa mara nyingine Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa imepoka demokrasia ya Wakenya kwa kumtangaza Kenyatta kuwa mshindi katika uchaguzi aliosema uligubikwa na ukiukwaji wa kanuni na taratibu.
Pamoja na kuweka wazi mpango wake huo wa kupinga matokeo ya uchaguzi huo mahakamani, Odinga ilibidi asubiri agizo la Mahakama la kuzitaka mamlaka zilizotajwa kuwa na nyaraka za kumwezesha kuwasilisha rufani yake ikiwemo Kampuni ya Simu ya Safaricom na IEBC kutoa nyaraka zitakazotumiwa na Odinga kama vielelezo vya kukiukwa kwa kanuni za uchaguzi huo.