Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

'BWANA MAPESA' MGONJWA, ALAZWA HOSPITALI YA AGA KHAN...

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Salma, wakimjulia hali Mheshimiwa John Cheyo hospitalini alikolazwa kwa matibabu jana. Katikati ni mjukuu wa Cheyo, Gabriel.
Mbunge wa Bariadi Magharibi, John Cheyo (UDP), amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, tangu Jumapili iliyopita.

Taarifa kutoka Ikulu ilieleza kuwa, Rais Jakaya Kikwete juzi usiku alimtembelea na kumjulia hali Mbunge huyo, ambapo pia  alizungumza naye kwa muda.
Rais alimpa pole Cheyo na kumtakia apone haraka, ili aendelee na shughuli zake za uwakilishi wa wananchi.
Mwandishi aliyefika hospitalini hapo, aliambiwa hali yake inaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa siku alipofikishwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa binamu wa mbunge huyo, Ecoles Msuya, hali ya Cheyo inaendelea kuimarika siku hadi siku na hivyo kutoa matumaini ya kuruhusiwa mapema.
"Kwa sasa amejipumzika hawezi kuzungumza juu ya suala lolote, ni vyema akaachwa hadi kesho pengine anaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kusema lolote, hali yake inaendelea vizuri na hiyo ni kauli aliyoniambia niizungumze," alisema Msuya.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah  jana alikwenda kumjulia hali mbunge huyo na kumweleza mwandishi kwamba hali ya Cheyo inaendelea vizuri kutokana na majibu aliyoyapata kutoka kwake.
"Suala la ugonjwa wa mtu ni jukumu lake mwenyewe kulielezea, isipokuwa nilipomuona na kumjulia hali alinieleza kuwa anaendelea vizuri na hata nilipomuona nimethibitisha hivyo," alisema Dk Kashililah.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles