Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

KAMATI ZA BUNGE ZAVUNJWA KWA KUKITHIRI RUSHWA...

$
0
0
Ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Kamati za Bunge zimetangazwa, ambapo wajumbe wa kamati mbili zilizowahi kutuhumiwa kwa rushwa, wamesambaratishwa.
Kwa mujibu wa orodha mpya ya wajumbe wa kamati hizo iliyotolewa jana na Ofisi ya Bunge, Kamati ya Hesabu za Serikali na ya Nishati na Madini zilizopata kutuhumiwa kwa rushwa, zimesambaratishwa.
Mbali na hatua hiyo, kwa maana ya wajumbe wake kusambazwa katika kamati zingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amepangwa kupambana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, John Cheyo.
Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa na wajumbe 25 ambao baadhi walituhumiwa kupokea rushwa ili kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, imebakiwa na wajumbe watatu wa zamani.
Katika Kamati iliyopita, wajumbe walikuwa Selemani Zedi, aliyekuwa Mwenyekiti, Diana Chilolo, Makamu Mwenyekiti na John Mnyika.
Wengine walikuwa Yusuph Haji Khamis, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yussuph Nassir, Christopher ole Sendeka, Dk Festus Limbu, Shaffin Sumar, Lucy Mayenga na Josephine Chagula.
Wengine ni Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Nchambi Suleiman, Kisyeri Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata, Mbarouk Ali, Athuman Mfutakamba na Pamela Palangyo.
Kwa sasa inaundwa na wajumbe wachache kuliko iliyopita akiwamo Victor Mwambalaswa, Saleh Pamba, David Silinde, Martha Mlata, Devotha Likokola, Raya Khamis,  Murtaza Mangungu na Juma Njwayo.
Wengine ni Jerome Bwanausi, Richard Ndassa, Anne Kilango,  Herbert Mntangi, Shaffin Sumar, Yussuf Haji Khamis na Riziki Lulida na wa zamani Chagula, Charles Mwijage na Mariam Kisangi.
Kamati nyingine iliyosambaratishwa ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambapo  wajumbe walioteuliwa  ni  Deusderius Mipata, Filikunjombe, Asha Jecha na Lucy Owenya.
Wengine ni Esther Matiko, Cheyo, Zitto, Zainab Vulu, Ally Keissy, Zainab Kawawa, Kheri Ali Khamis, Faida Mohamed Bakari, Ismael Aden Rage, Modestus Kilufi, Abdul Marombwa, Gaudence  Kayombo, Kombo Khamis Kombo na Catherine Magige.
Wajumbe wa zamani walikuwa Augustine Mrema, aliyekuwa Mwenyekiti, Iddi Azzan, Makamu Mwenyekiti; Riziki Saidi Lulinda, Zabein Mhita na Godfrey Zambi.
Wengine ni Subira Mgalu, Hasnain Murji, Susan Kiwanga, David Kafulila, Omary Badwel, Abdul Mteketa, Tauhida Nyimbo, Joseph Selasini, Kuruthum Mchuchuli, Maida Abdalah, Dk Cyril Chami.
Kamati hiyo, katika mikutano ya Bunge iliyopita, wajumbe wake walituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa huku mjumbe wake ambaye ni Mbunge wa Bahi, Badwel, akipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kupokea rushwa na kesi yake bado inaendelea.
Aidha, katika orodha hiyo mpya, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto na Makamu wake, Filikunjombe, wameingizwa kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali ambayo aliyekuwa Mwenyekiti wake, Cheyo anaendelea kuwa kwenye Kamati.
Kutokana na mabadiliko hayo, katika uchaguzi wa viongozi wa kamati hizo unaotarajiwa kufanyika leo, mchuano mkali utakuwa baina ya Zitto na Cheyo katika nafasi ya uenyekiti kutokana na taratibu zilizopo kuonesha kuwa Kamati hiyo, huongozwa na mbunge kutoka chama cha upinzani.
Aidha, katika orodha hiyo inaonesha kuwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Kilango, ameondolewa kwenye Kamati hiyo na kuingizwa Kamati ya Nishati na Madini ambayo wajumbe wake wa awali 25, takribani wote isipokuwa wanne wamehamishiwa kamati zingine.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles