![]() |
Patricia Murphy (katikati) kabla ya kuangukia kwenye ulevi na kulia akiwa amelazwa hospitalini. |
Kiasi cha juu kabisa cha pombe kilichopendekezwa kutumiwa kwa wanawake ni kati ya uniti mbili na tatu kwa siku, na kisizidi uniti 14 kwa wiki.
Hivyo inashangaza mno kwamba Patricia Murphy - ambaye alikunywa hadi uniti 350 kila wiki kwa miaka 25 - mwishowe akaishia kulazwa hospitali akiishi kwa msaada wa mashine ya kusaidia maisha huku akisumbuliwa na matatizo ya ini, au kwamba sasa anasubiri kuelezwa kama atalazimika kupandikiziwa ini jingine.
Patricia, mwenye umri wa miaka 45, anaishi huko Chessington, Surrey, na amekuwa mtulivu kwa miezi saba. Akijihisi mwenye bahati kuendelea kuwa hai, ofisa mauzo huyo wa zamani sasa anatamani kusimulia kisa chake, kwa nia ya kuwaonya wanawake wengine kuhusu hatari za pombe, kinywaji halali ambacho kimeangamiza maisha yake.
Patricia alianza kunywa pombe wakati alipokuwa na miaka 17, baada ya kumaliza shule akisomea kuwa ofisa mauzo.
Kawaida mwenye aibu, lakini ulevi ulimfanya ajihisi mwenye kujiamini kati ya wenzake, na mara akawa anakunywa vilevi 10 vya brandi na soda siku za mwishoni mwa wiki.
Alipoanza kufanya kazi kwenye kampuni ya kuuza kompyuta alikuwa akinywa pombe kila siku usiku na wenzake - wakati mwingine hadi lita moja ya pombe ya brandi.
Akiwa na miaka 28, wazazi wake wote walifariki wakipishana miezi mitano, na pombe ikawa kitu pekee ambacho kingeweza kumwondolea huzuni.
"Pombe ilisitisha machungu hayo. Nilikunywa glasi ya mvinyo asubuhi, kisha nyingine zaidi siku nzima. Nilikuwa nikiishi peke yangu hivyo hakukuwa na mtu wa kunizuia. Nilifukuzwa kazi sababu ya ulevi.
"Nilikuwa mlevi mno kiasi cha kusahau kurudi na kushindwa kujizuia kabisa. Kaka na dada zangu waliniambia nipunguze, lakini niliwapuuza, niliaibika kwa jinsi maisha yangu yalivyobadilika lakini sikuacha."
Muda mfupi baadaye akawa anakunywa chupa tano za mvinyo kila siku, na kuamka usiku wa manane akitweta na kutetemeka. Alitumia fedha zake zote za mafao kununulia pombe, na kutumia siku nzima akitazama televisheni na kujihisi kufadhaika.
Wakati, alipofikisha miaka 35, akapata mpenzi Graham, sasa ana miaka 42, kwenye baa, hakuweza kuficha ulevi wake uliopindukia: Graham, mhandisi, alikuwa hanwi kilevi chochote.
Mama wa Graham alikuwa mlevi, na akamwongoza Patricia kwenda kurekebishwa tabia - lakini mara baada ya kutoka hapo akaelekea moja kwa moja na kuagiza chupa ya mvinyo.
Licha ya kuhudhuria mikutano kadhaa ya kuachana na ulevi na kukubali kwenda katika mafunzo ya kubadilisha tabia mara mbili kwa miaka minne iliyofuata, Patricia alionana na daktari Novemba mwaka jana - baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa Graham - na alielezwa kwamba ini lake kuwa limeharibika kwa kiasi kikubwa.
Alipelekwa hospitali akiwa hajitambui: wakati akiwa kwenye mashine ya kusaidia maisha, Grahama aliambiwa kuna nafasi asilimia tano tu ya mpenzi wake huyo kupona. Mchungaji akafika kwa ajili ya kumwongoza sala ya mwisho.
Lakini mbali na hatari zote - na baada ya wiki 10 za kukaa hospitalini hapo - Patricia aliruhusiwa kwenda nyumbani. Licha ya mateso yake, kitu cha kwanza alichofanya baada ya kuruhusiwa ilikuwa kununua mvinyo. Kwa bahati, alikerwa mwenyewe kuthubutu kufanya hivyo, na amekuwa mtulivu tangu hapo.
"Kwa sasa, madaktari wanafurahishwa na maendeleo yangu, lakini maisha yangu kwa ujumla yatakuwa yameathirika. Ini langu linatia mashaka, wakati wowote litaacha kufanya kazi."
Uchunguzi utakaofanywa Oktoba utaamua kama Patricia anahitaji kupandikiziwa ini jingine au la.
"Najihisi mwenye hatia mno kuhusu machungu niliyowasababishia wote walio karibu nami, nitajuta milele kwa kutokuwa na kazi au watoto."