Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

MTALII ABAKWA NA WANAUME WATATU, AKIWAMO BABU WA MIAKA 70...

Mtalii wa kike kutoka Uingereza amebakwa na kundi la wanaume mita chache tu kutoka mahali alipofikia kwa ajili ya mapumziko alipokuwa akiishi na rafiki yake wa kiume huko Costa del Sol, nchini Hispania, imedaiwa.
Msichana huyo mwenye miaka 31 alishambuliwa na wanaume watatu mapema Jumapili asubuhi wakati akitembea, peke yake, kutoka kwenye matembezi ya usiku katika mji wa kusini wa Benalmadena.
Gazeti la La Opinion de Malaga limeripori wawili hao walikuwa kwenye sherehe katika eneo maarufu la Puerto Marina, lakini msichana huyo aliamua kurejea kwenye ghorofa hilo mapema Saa 7 usiku baada ya kutokea malumbano kati yao.
Alisimamisha taksi lakini muda mfupi alishuka humo. Dereva alimlazimisha kushuka garini, hivyo akatembea kwa miguu sehemu iliyobaki ya safari yake.
Kwa mujibu wa ushahidi wake, alikuwa akitembea kwenye hadhaki, barabara ya chini N-340 yenye pilika nyingi, na hiyo ikamfikisha ufukwe maarufu wa Carvajal Beach, ambapo alijongelewa.
Wanaume watatu, walioonekana kama Waarabu, walimsimamisha.
Mmoja alikuwa na umri wa miaka takribani 70, na wengine wawili walionekana dhahiri kuwa vijana.
Wanadaiwa kuwa walimkokota, kabla ya kumpeleka kwenye eneo lililojitenga. Mmoja wa wanaume hao alimshikilia chini huku wengine wakitumia fursa hiyo kumbaka.
Baada ya shambulio hilo, alitembea kurudi kwenye makazi yake lakini hakuweza kuingia au hata kuwasiliana na rafiki yake wa kiume sababu alikuwa ameibiwa kila kitu chake.
Mpitanjia aliwasiliana na polisi baada ya kumkuta msichana huyo akiwa ameanguka chini, nje ya nyumba yake majira ya saa 9 alfajiri.
Alichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Centro Hospitalario de Alta Resolución de Especialidades kwa matibabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles