![]() |
Moja ya mitaa ya mkoani Mara. |
Ukatili mpya wa kijinsia unaojulikana kama ‘Memory Card’ umezuka mkoani Mara na kusababisha mauaji ya wanawake zaidi ya 14 katika kipindi cha kuanzia Desemba mwaka jana hadi Julai, mwaka huu.
Ukatili huo huhusisha ukataji wa kichwa na sehemu ya uke ili kuwawezesha wauaji kuchukua damu na kiungo cha uke na kuvipeleka kwa waganga wa kienyeji ili wapate dawa ya kupata utajiri kwenye madini na uvuvi wa samaki.
Hayo yalielezwa na wanawake mbalimbali wakati wakizungumza kwenye mdahalo wa kupinga ukatili wa wanawake na watoto wa kike uliofanyika katika Kijiji cha Bisumwa, wilayani Butiama mkoani Mara ambapo walisema mauaji hayo yanaongozwa na kundi la watu wanaojiita Makirikiri.
Katika mdahalo huo ulioandaliwa na Shirika la Kutetea haki za Wanawake na Watoto wa Kike la Kivulini kupitia Kampeni yake ya Tunaweza, wanawake hao walisema ukatili huo umekuwa ukifanywa na watu walio karibu na familia zao.
Akizungumza katika mdahalo huo Msaidizi wa Kisheria, Maria Michael alisema wauaji hao wamekuwa wakitafuta viungo vya wanawake katika kuwapatia mali nyingi hasa katika madini na uvuvi.
Alisema hali hiyo ambayo inachangiwa na mila na desturi ya utoaji wa mahari, wanaume hujiona wanawamiliki wanawake na hivyo kwenda kwa waganga ambao huwadanganya kuwa wakipeleka viungo hivyo watafanyiwa dawa na kuwa matajiri.
“Matukio hayo ya mauaji ya wanawake na kukatwa sehemu zao za siri pamoja na kichwa yamerudisha nyuma uchumi kutokana na wanawake kuhofia kutoka ndani ya nyumba na kwenda shamba au katika shughuli nyingine za kuwaongezea kipato,” alisema.
Alisema swali wanalopaswa kujiuliza ni kwa vipi viungo vya wanawake viwaletee wanaume utajiri kama si imani potofu wanayodanganywa na waganga wa kienyeji, na kama ingekuwa ndivyo mbona hawajawahi kuona wananunua ndege kwa kutumia viungo vya wanawake?
Alisema vitendo hivyo vya ukatili vimesababisha wanawake kuungana katika makundi wakati wanapokwenda shambani kulima ili wasidhuriwe pamoja na wanafunzi wanapokwenda shuleni.
Naye Elizabeth Samson akizungumzia nini kifanyike aliwataka viongozi wa Serikali za Mitaa wabadilike wakati wanapotoa huduma kwa jamii kwa vile baadhi ya wanaofanyiwa ukatili na kupeleka malalamiko hayo huko huzungushwa na kudaiwa fedha.
Aliongeza kuwa pia polisi wamekuwa wakichukua muda mrefu kupeleka kesi mahakamani na zikifikishwa hubadilishwa na kuwafanya wenye fedha kushinda kesi hizo.
Akielezea hatua zilizochukuliwa na Shirika la Kivulini, Ofisa Sera na Utetezi, Khadija Liganga alisema kwa kuwa mauaji hayo yamekuwa yakifanyika kwa siri polisi walithibitisha kuyafuatilia kwa karibu ili kubaini maeneo yanayoongoza kwa mauaji hayo.
Alisema pia wamekuwa wakiwaelimisha wanawake kutoa taarifa pale wanapobaini kutokea kwa tukio la ukatili na kuhakikisha wanatembea katika makundi ambapo kundi la Makirikiri linalotajwa kuhusika na mauaji hayo haliwezi kuwavamia wanapokuwa zaidi ya mtu mmoja.
Aliyataja maeneo walipouawa wanawake hao kuwa ni Butiama walikouawa wanawake wanane, Musoma Mjini wanawake watatu, Makoko mwanamke mmoja na Rwamlimi alikouawa mwanafunzi mmoja aliyekuwa akitoka Musoma Mjini kwenda Butiama.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula alisema kwa hivi sasa matukio hayo yamedhibitiwa na serikali kupitia Kamati zake za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mkoa na kuimarishwa kwa Ulinzi Shirikishi.