![]() |
KUSHOTO: Christian Benitez akifanya vitu vyake uwanjani. KULIA: Chritian Benitez. |
Mshambuliaji wa zamani wa Birmingham City, Christian Benitez amefariki ghafla kwa kile kinachodhaniwa matatizo ya moyo akiwa na umri wa miaka 27.
Kifo cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador kimekuja wiki chache tu baada ya uhamisho wake uliogharimu Pauni za Uingereza milioni 10 kwenda klabu ya El Jaish ya Qatar akitokea timu ya Club America ya Mexico.
Huku wanasoka sehemu mbalimbali duniani wakituma salamu za rambirambi katika mtandao wa Twitter, Shirikisho la Soka la Ecuador limebainisha alikimbizwa hospitali juzi kutokana na 'maumivu makali ya tumbo' kabla ya kufariki kwa ugonjwa wa moyo.
El Jaish pia ilitoa taarifa kuthibitisha habari hizo. Ilisema: "Klabu inapenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya mchezaji huyo.
"Benitez hivi karibuni alijiunga na timu hii kutoka Club America kwa misimu mitatu.
"Mchezaji huyo alishiriki kwa mara ya kwanza katika timu hii kwenye mechi ya juzi dhidi ya Qatar Sports Club katika Kombe la Sheikh Jassem bila kulalamika matatizo yoyote ya kiafya.
"Kifo chake cha ghafla ni mshituko mkubwa kwa kila mtu kwenye benchi la ufundi na wafanyakazi wa utawala.
"Alikuwa mchezaji ambaye kwa kipindi kifupi alichokuwa hapa alichukuliwa kama mtu mwenye hamasa ya hali ya juu."
Benitez ambaye alipachikwa jina la utani 'Chucho', alikuwa akicheza kwa mkopo St Andrew's msimu wa 2009-10, na kuchezea kikosi hicho cha Blues mechi 36. Alishinda mataji 58 akiwa na Ecuador, zikiwamo mechi kadhaa za Kombe la Dunia mwaka 2006.