Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

IMEBAINIKA: USAIN BOLT HUZALISHA NISHATI MARA 50 ZAIDI YA RISASI INAPOFYATUKA...

$
0
0
Mwanariadha Usain Bolt akiweka pozi lake maarufu baada ya kushinda mbio.
Bingwa wa Olimpiki Usain Bolt anazalisha nishati mara 50 zaidi ya ile ya risasi iliyofyatuka kutoka kwenye bunduki wakati wa moja ya mbio zake za mita 100 alizovunja rekodi, wanasayansi wamebainisha.

Wanasayansi wanaotafiti siri hizo za mafanikio ya Bolt wametangaza matokeo hayo baada ya utafiti wa kina wa ushiriki wa mwanariadha huyo wa Jamaica kwenye mbio za mita 100 wakati wa Mashindano ya Ubingwa wa Dunia mjini Berlin mwaka 2009.
Waligundua kwamba alizalisha nishati ya juu ya 81.58kJ - kulinganisha na 1.6kJ inayozalishwa na risasi wakati ikitoka kwenye bunduki ya Magnum yenye kipenyo cha 0.44.
Pia walipiga hesabu za alipofikisha kasi ya juu kabisa ya maili 27 kwa saa wakati wa mbio hizo.
Lakini kwa bahati mbaya risasi - inaweza kufikia kasi ya maili 1,000 kwa saa - umbile kubwa la Bolt la futi 6 na inchi 5 linamaanisha zaidi ya asilimia 92 ya nishati yake iliyomezwa katika mapambano kukinzana na upepo.
Watafiti hao waligundua alilazimika kuzalisha kiasi 'kisicho cha kawaida' cha nguvu kuweza kufikia muda wa rekodi yake ya dunia katika mbio za mita 100 - na kwa sababu ni mrefu mno hutumia elimumwendo kidogo zaidi kuliko wastani wa binadamu.
Walifanya ugunduzi huo baada ya kuzingatia mwinuko wa njia za kukimbilia za Berlin, joto wakati wa mbio hizo na mwili wa Bolt mwenyewe kwa ujumla.
Bolt alifikia nguvu ya mwisho ya wati 2,619.5 - nguvu farasi ya 3.5 - ndani ya sekunde 0.89 wakati alipokuwa tu nusu ya kasi yake ya juu, ambayo inaonesha athari ya mburuto huo katika mwendo wake.
Watafiti hao, kutoka Chuo Kikuu cha National Autonomous cha Mexico, alidai milinganyo yao inaweza kutumika kupiga hesabu athari za upepo mkia, ambao unaweza kutofautiana kati ya mbio na kwa umuhimu kupunguza mida ya kukimbia.
Walilinganisha muda wa Bolt huko Berlin na muda wa rekodi yake iliyopita ya dunia ya sekunde 9.69, aliyoweka kwenye Olimpiki za Beijing mwaka mmoja kabla.
Mjini Beijing, Bolt alikuwa akikimbia bila upepo mkia, lakini mjini Berlin kulikuwa na upepo mkia wa mita 0.9 kwa sekunde.
Kwa mujibu wa milinganyo ya watafiti hao, Bolt angeweza kufikia muda wa taratibu mjini Berlin kama hakungekuwa na upepo mkia, lakini bado angeweza kuvunja rekodi yake ya dunia ya Beijing - wanabashiri kwamba angeweza kufikia muda wa sekunde 9.68.
Mahesabu hayo katika utafiti huo yalipimwa kwa usahihi kwa kuingiza data za kitafiti za maisha halisia kwenye milinganyo hiyo.
Namba hizo zilitoka kwa chombo cha kupima kasimwelekeo cha Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF), ambacho kilirekodi nafasi ya Bolt na kasi katika kila moja ya kumi ya sekunde wakati wa mbio za mwaka 2009 mjini Berlin.
Usain Bolt alikuwa mjini London kwenye bustani ya Olimpiki jana kushiriki katika kumbukumbu ya michezo hiyo kuadhimisha mwaka mmoja tangu michezo iliyofanyika London mwaka 2012.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles