![]() |
Penny Dane katika pozi tofauti. |
Sajenti wa polisi ameacha kazi baada ya uchunguzi kukuta picha zake akiwa uchi kwenye kompyuta yake ya kazi na mitandao ya ngono ambayo anadaiwa alikuwa akitazama wakati wa kazi.
Sajenti huyo wa Idara ya Polisi ya Daytona Beach, Penny Dane alihifadhi picha zake akiwa amekaa pozi zinazohamasisha ngono akiwa amevalia sare zake katika kompyuta ya kazi na kutuma picha zake za uchi katika mitandao ya ngono akiwa kazini, uchunguzi huo umebaini.
Mama huyo wa watoto wawili, ambaye ametumikia kikosi hicho kwa miaka 17, ameacha kazi baada ya ugunduzi huo, imeripotiwa.
Uchunguzi huo wa ndani ambao ulifanyika pale Dane alipofungua madai dhidi ya ofisa mwingine na ikalazimika kompyuta yake kuchunguzwa kama sehemu ya madai hayo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya ndani, Dane alitumia kompyuta zote zilizotolewa kuhifadhi zaidi ya picha cha uchi 270 wakati anapokuwa kazini na kuwasimamia maofisa wengine, imeripotiwa.
Maofisa walidai kwamba Dane alitumia michezo ya kwenye mtandao, ambapo watazamaji waliweza kutazama ngono moja kwa moja, wakati wa kazi.
Maofisa waligundua picha 177 katika kompyuta ya ofisini kwa Dane na picha 97 kwenye kompyuta yake ya mapajani ndani ya gari lake la doria, imeripotiwa.
Takribani picha 23 kati ya hizo zilikuwa za Sajenti huyo mwenyewe, ilidaiwa.
Mkuu wa Idara ya Polisi ya Daytona Beach, Mike Chitwood alidai kwamba Dane kwa makusudi alizima kifaa cha kusakia kwenye gari lake wakati anapoingia kwenye mtandao na kushughulikia picha hizo za ngono.
Lakini Sajenti huyo alidaiwa kutetea vitendo vyake, akisema kwamba hakuwahi kuacha kupokea simu sababu eti alikuwa akichungulika na vitendo vyake hivyo haramu na majukumu yake ya kusimamia sheria.
Sajenti Dane alidaiwa kuwaeleza wachunguzi alikuwa na uwezo wa kufanya majukumu zaidi ya moja wakati akiwa kazini, na hakuwahi kuacha kupokea simu wakati akishughulikia picha hizo, imeripotiwa.
Chifu Mike Chitwood amesema ofisa huyo hakufukuzwa kazi lakini suala hilo limeichafua Idara ya Usimamizi wa Sheria ya Florida, imeripotiwa.
"Amepoteza sifa na haki yake ya kuwa ofisa wa polisi," alisema Chitwood.
"Tutamnyang'anya leseni yake hivyo hawezi kamwe kuwa askari tena. Kutokuwa askari popote pale katika Jimbo la Florida."
Chifu Chitwood hakupatikana kuzungumzia hilo pale alipotafutwa na mwandishi.