![]() |
Eneo la Parachinar ambako alihamishiwa Anwar. |
Mwanajeshi wa Pakistan amepigwa mawe hadharani hadi kufa ikiwa ni amri ya mahakama ya kijadi kwa kuwa na mahusiano na mwanamke wa kawaida, imedaiwa jana.
Anwar Din mwenye miaka 27, mzaliwa wa Punjab, alipewa uhamisho kutoka mkoa wa Kurram ulioko kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo mwaka jana kwenda eneo la Parachinar ambako alikutana na Intizar Bibi mwenye miaka 19, kwenye sehemu yake ya kazi karibu na nyumbani kwa binti huyo.
Wawili hao waliangukia kwenye mahusiano ya kimapenzi, vyanzo vya habari vya kabila hilo na maofisa wa serikali walisema, na alijaribu kutoroka naye wakati alipohamishiwa baadaye kwenye mkoa wenye ugomvi wa Kashmir.
Haikuweza kufahamika mara moja ushahidi gani uliwasilishwa, wowote, wa kimapenzi.
"Msichana huyo aliondoka nyumbani kwake Jumatatu na kukutana na Anwar Din wakati wanakijiji walipowaona," alisema Munir Hussain, mkuu wa jigra, au mahakama ya kimila, ambayo ilimhukumu kifo Anwar.
"Tulimpeleka binti rumande na kumchukua mvulana huyo kwenye eneo la makaburi ambako alipigwa mawe hadi kufa na kuzikwa."
Anwar aliuawa Jumatatu, aliongeza. Ofisa mmoja wa Serikali, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema jigra ilimhukumu mwanamke huyo lazima apigwe hadi kufa. Haikuweza kufahamika mara moja kama hukumu hiyo tayari imeshatekelezwa.
Jeshi la nchi hiyo halikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo.
Kurram, sehemu pekee kubwa ya mpakani mwa Pakistan isiyofuata sheria ambayo ina wakazi wengi wa kabila la Shi'ite, imeathiriwa mno na vurugu kati ya makabila ya Sunni na Shi'ite. Wanaopingana na mawazo ya Shi'ite kutoka Taliban na al Qaeda wameendeleza miaka kadhaa ya mapigano ya umwagaji damu.
Bibi anatokea kabila na Shi'ite wakati Anwar ni kutoka kabila la Sunni, Hussain aliongeza.
Hussain alisema kwamba mahakama hiyo ya jigra pia iliomba kwamba askari mwingine wa Pakistani, Saif Ullah, akabidhiwe kwa kuwasaidia wawili hao kuonana na kuratibu mipango ya kutoroka kwao.
"Jeshi lipo hapa kwa ulinzi wetu lakini endapo wanajiingiza katika vitendo kama hivyo hatutaruhusu wakae hapa," Hussain alisema.
"Haya ni matusi kwa mila za kabila letu. Tutachukizwa dhidi ya hili."