Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

NJIWA MWENYE HIRIZI AZUA KIZAAZAA OFISI ZA TAZARA MBEYA...

$
0
0

Njiwa aliyevishwa shanga na hirizi shingoni huku akiwa amebeba ujumbe wenye onyo kali juzi alisababisha taharuki kubwa katika ofisi za Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) zilizopo jijini Mbeya.

Ni baada ya kugundulika kuwa njiwa huyo alikuwa ametua katika moja ya vyoo vilivyopo kwenye ofisi hizo ndipo wafanyakazi walijikuta kwenye wakati mgumu na baadhi yao kulazimika kuzikimbia ofisi zao.
Saa mbili asubuhi juzi, mtumishi mmoja wa Tazara alibaini uwepo wa njiwa huyo na hapo ndipo mjadala mkubwa ukaibuka na kuvuta hisia za watu wengi wakiwemo wakazi wa maeneo ya jirani na ofisi hizo walioamua kufika kujionea.
Waandishi wa habari walikuwa ni miongoni mwa mashuhuda waliomuona njiwa huyo wa rangi nyeusi akiwa akiwa nyuma ya choo cha kiume kilichopo jirani na ofisi ya mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi shingoni iliyozungushiwa shanga mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni nyekundu, njano na nyeupe.
Hoja nzito ilihusu ujumbe uliokuwa kwenye barua aliyowasilisha njiwa huyo mahali hapo ambapo baadhi ya watumishi walionesha kumhisi mtumishi mmoja aliyefukuzwa  kazi hivi karibuni kwenye mamlaka hiyo kutokana na ubadhirifu.
Barua hiyo ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha mbili za Kiswahili na Kiarabu, ambapo katika maandishi ya Kiswahili yalisomeka ‘Naomba majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini’ huku ikitaja orodha ya majina ya viongozi watatu wa wa shirika hilo.
Ujumbe huo ulioonekana kuandikwa kwa mkono na kukolezwa kwa wino mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa mbele kulikuwa na maandishi yakiwa ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo.
Mwajiri wa Shirika hilo Kanda ya Mbeya, Mchaba Mgweno, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba waliobaini ni wahudumu wa usafi.
Mgweno aliongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwaarifu wafanyakazi wenzake ambao walikusanyika na kumshuhudia njiwa huyo mweusi akiwa amedhoofika huku akiwa na barua hiyo yenye vitisho. 
“Baada ya kushuhudia hali hiyo, tuliamua kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo ndani ya eneo la ofisi za shirika letu, ambapo waliichukua barua hiyo na baadhi ya wafanyakazi hao wakienda kutoa maelezo kituoni hapo.
“Kwetu sisi tunaona hali hii si ya kawaida, ila kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote kwa kuwa hata mimi tukio hili limeniweka katika wakati mgumu na nimeshindwa kuendelea na majukumu yangu,” alisema Mgweno.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles