Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

MFANYAKAZI KIKONGWE ZAIDI DUNIANI? ANA UMRI WA MIAKA 92 NA BADO YUKO KAZINI...

$
0
0
Sara Dappen.
Mwanamke mmoja kikongwe wa Iowa anaweza kuwa mfanyakazi wa mgahawa wa McDonald's mwenye umri mkubwa zaidi, na bado anaipenda kazi hiyo akiwa na umri wa miaka 92.

Sara Dappen alizaliwa mwaka 1920, alikuwa sehemu ya wahitimu wa darasa la mwaka 1938 kwenye Sekondari ya Juu ya Story City na darasa la mwaka 1942 katika Chuo Kikuu cha Iowa.
Siku hizi ijapokuwa utamkuta akigeuza baga katika mgahawa wa McDonald's tawi la Iowa, ambako amefanya kazi kwa miaka mitano iliyopita.
"Nilifikiri ilikuwa inapendeza zaidi kuendelea kuzunguka eneo hili kuliko kupandisha na kushusha kwenye mtaa huu, na hii inaniepushia kubweteka," alisema.
Bibi Dappen ni mkubwa kwa miaka minne zaidi ya mfanyakazi mzee kabisa wa mgahawa huo nchini Uingereza, Bill Dudley mwenye miaka 88, ambaye huwasalimu wateja na kufuta vumbi kwenye meza katika sehemu ya chakula cha chap-chap huko Mold, Clwyd.
Naye pia husafisha meza na kuzikunja baada ya wateja kuondoka, lakini alisema kitu anachopendelea zaidi kufanya ni kuongea na watu ambao wanafika kwenye mgahawa huo.
Wote Bibi Dappen na Dudley, lazima wafuate zamu zao kwenye sehemu hiyo ya chakula cha chap-chap ili waweze kuongeza mafao yao, lakini kamwe haiwezi kuwa zaidi ya nyongeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles