![]() |
Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma. |
Licha ya viongozi wa juu wa Chadema kukataza wabunge wao kuhojiwa, baadhi yao wamesalimu amri kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa kuitikia mwito wa kwenda kuhojiwa kuhusu vurugu zilizotokea mkutano uliopita wa Bunge.
Vyanzo vilisema hadi jana, wabunge watano walishahojiwa; ambao kati yao, wanne ni wa Chadema na mmoja wa NCCR-Mageuzi.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ni miongoni mwa waliohojiwa.
Wengine wa Chadema ni wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; wabunge wa viti maalumu, Lucy Owenya na Muhonga Ruhwanya.
Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Upinzani, juzi akiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa, katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, alisema hakuna mbunge wa Chadema atakayekwenda kuhojiwa.
Alitoa sababu ya mgomo huo kwamba ni mtazamo wao kuwa Kamati hiyo si halali. Mbunge wa NCCR-Mageuzi aliyehojiwa ni wa Kasulu Mjini, Moses Machali.
Akizungumza na mwandishi kuhusu kuhojiwa na Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi, Lissu alisema: “Sijahojiwa, huo ni uongo, nilikwenda kwenye Kamati hiyo Jumatatu nikawauliza naitiwa nini, tena kwa amri ya Polisi.
“Ndipo wakanipa hati ya kuitwa, lakini nikawajibu palepale kuwa siwezi kuwajibu chochote kuhusu mwito huu na kiutaratibu ukipewa hati hiyo una haki ya kusubiri siku tatu, ili ujiandae,” alisema.
Alisisitiza msimamo wa wabunge wa Chadema kuwa ni kutotii amri ya kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kwamba hawatalazimika kwenda mbele ya Kamati kwa pingu, kwa kuwa hakuna mbunge aliyepewa hati ya kuitwa zaidi ya amri ya Polisi, wakati yeye ameshapokea hati hiyo.
Kuhusu kauli ya Naibu Spika, Job Ndugai kuwa iwapo wabunge hao watakaidi mwito huo wa kuhojiwa na Kamati watalazimika kupelekwa kwa pingu, alisema hilo haliwezekani kutokana na utaratibu uliotumika kuwaita.
“Kisheria ukiitwa kwa kutumiwa hati, ni lazima utii na usipotii ndipo unalazimika kwenda kinguvu na Polisi, lakini hakuna mbunge ambaye hadi sasa amepewa hati ya kuitwa zaidi ya amri ya Polisi, na hiyo hata sijui sheria inasemaje iwapo mtu asipokwenda,” alisisitiza Lissu.
Kama ilivyo kwa Lissu, pia Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa, alikiri kwenda mbele ya Kamati hiyo lakini kwa kusisitiza kwamba hakwenda kuhojiwa, bali aliitika ujumbe aliopewa na Polisi Iringa uliomtaka afike kwenye kikao cha Bunge.
Mchungaji Msigwa alisema: “Sijahojiwa. Nilikwenda pale kuwakatalia … kweli nilifika, lakini niliwaambia hawana uhalali. Nilisema hawana uhalali wa kunihoji kwa sababu wameniita kwa kutumia ujumbe wa Polisi na wala haikuwa hati maalumu ya kuitwa kuhojiwa.”
“Anayetakiwa kuleta hati ya kuitwa ni polisi au karani wa Bunge, lakini mimi nilipewa ujumbe na polisi kwamba natakiwa kuonekana kwenye kikao cha Bunge na mimi kama raia mwema nikaitika hilo, lakini sikwenda kuhojiwa,” alisisitiza.
Mbunge huyo aliendelea kusisitiza, kwamba haitambui Kamati hiyo akisema ile halali wanatarajia itaundwa wiki ijayo. “Hii ni Kamati feki, halali tunatarajia kuipata wiki ijayo,” alisema.
Owenya alikanusha kuhojiwa na Kamati hiyo akisema: “Mimi, sijahojiwa. Kwanza niko Moshi…wabunge hawajahojiwa.” Mbunge Ruhwanya alipopigiwa simu, hakuzungumzia suala hilo zaidi ya kusema yuko sehemu ambayo hapatakiwi kuzungumza na simu.
Wakati huo huo, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR -Mageuzi), ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo ambaye yumo kwenye orodha ya watuhumiwa 28 wanaopaswa kuhojiwa na Kamati hiyo.
Akizungumza na mwandishi jana, Kafulila alisema ingawa hajapewa barua rasmi zaidi ya taarifa aliyopewa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, alisisitiza kwamba atakwenda kuhojiwa.
“Sijapewa barua rasmi labda leo (jana) au kesho (leo) … nitakwenda kuhojiwa. Mimi sioni kosa lolote, sioni kitu ambacho nitashindwa kujibu. Naona ni nafasi nzuri ya kueleza kile ninachoamini kuhusu uendeshaji wa Bunge,” alisema Kafulila.
Alisema hana taarifa yoyote kutoka chama chake wala kambi ya Upinzani inayomkataza kwenda kuhojiwa. Hata hivyo, alisema kwa kuwa hajapata barua, hajui siku rasmi ya kuhojiwa.
Akielezea nafasi yake katika Kamati hiyo inayoongozwa na Ngwilizi, Kafulila alisema:“Nimejumuishwa kwenye makosa. Kwa hiyo kesi inanihusu siwezi kuwa hakimu katika kesi inayonihusu.” Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inajumuisha wajumbe 18 wakiwamo makatibu wawili.
Baada ya Chadema kutangaza msimamo wake wa kutoruhusu wabunge wake kuhojiwa na Kamati hiyo, Ndugai alikaririwa na gazeti hili akisema iwapo watakaidi amri ya kuitwa, wahusika wako hatarini kufikishwa mbele ya Kamati wakiwa wamefungwa na pingu.
Mwenyekiti wa Kamati, Ngwilizi hakupatikana tangu juzi kutoa ufafanuzi wa malalamiko ya wabunge kwamba hawakupelekewa hati maalumu ya kuitwa, isipokuwa walitumiwa ujumbe kupitia Polisi, jambo ambalo wengi walisema hawakubaliani na utaratibu huo.
Chanzo cha wabunge hao kuhojiwa ni kutokana na vurugu zilizotokea bungeni katika Mkutano wa 10 wa Bunge katika kikao cha Februari 4.