Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

ACHINJWA SHINGO NA KUFA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA MBEYA...

$
0
0
Mtu mmoja amefariki dunia mkoani Mbeya baada ya kuchinjwa shingo na kufa kutokana na imani za kishirikina.
Aliyechinjwa hadi kufa amefahamika kwa jina la Nickson Mwazembe (65), mkazi katika kijiji cha Izyira wilayani Ileje.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Barakael Masaki alisema jana kuwa wauaji  hawajafahamika.
Alieleza kuwa tukio hilo lilitokea nyumbani kwa marehemu Machi 12, mwaka huu saa 8:00 usiku wakati Mwazembe akiwa amelala.
Masaki alisema wauaji  hao walimvizia Mwazembe akiwa amelala, wakati mkewe akiwa katika msiba nyumba ya jirani. Watu hao walimchinja kwa kutumia silaha, inayosadikiwa kuwa kisu au panga hadi kumuua.
Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuwasaka wauaji waliotokomea kusikojulikana baada ya kufanya mauaji hayo.
Alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikiana , ambapo baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakimtuhumu Mwazembe kuwa ni mchawi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles