Ndege ya United Airlines inayofanya safari zake Newark imebeba abiria ambaye alidhibitiwa baada ya kudai kwamba kila mtu kwenye ndege hiyo amelishwa sumu.
Mtuhumiwa huyo alidhibitiwa na abiria wengine waliokuwamo ndani ya ndege hiyo iliyokuwa katika safari ya masaa 14 kutoka Hong Kong.
Hakuna ushahidi kwamba abiria hao walikuwa wamelishwa sumu, imeripotiwa.
Ndege hiyo ya United Airlines yenye namba 116 ilipangwa kutua Saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Ndege wa Newark.
Maofisa wa FBI waliokwenda eneo la tukio wanatarajiwa kukutana na ndege hiyo kwenye uwanja huo wa ndege
Maosifa kutoka vyanzo vya habari za kisheria walieleza kwamba abiria huyo alisimama na kutoa taarifa hiyo masaa kadhaa yaliyopita na kwamba wafanyakazi wa ndege hiyo waliamua kuendelea na safari kuelekea Newark.