Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

MADINI YA URANI SASA KUANZA KUCHIMBWA RASMI RUVUMA...

$
0
0
Madini ya Urani.
Uchimbaji madini ya urani wilayani Namtumbo, Ruvuma unatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya Serikali kujiridhisha kuwa uchimbaji wake hauna madhara.

Imeweka wazi kuwa imejipanga kikamilifu kuchimba na tayari hadhari  ya kutosha imechukuliwa kuhakikisha hakuna madhara yanayojitokeza.
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati akizungumza na ujumbe wa nchi za  Umoja wa Ulaya (EU).
Alisema katika siku za karibuni baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa Serikali haijajipanga vya kutosha na uchimbaji wa madini hayo.
“Kauli hizi  hazina ukweli, kwani Serikali imefanya utafiti wa kina na kubaini kutokuwapo madhara kutokana na uchimbaji huo zaidi ya kunufaisha wananchi, Serikali na jamii na kuwa na tija kwa Taifa,” alisema.
Mkuu wa Idara ya Nyuklia ya EU, Pascal Daures, aliunga mkono kauli ya Waziri Muhongo kuwa  uchimbaji wa urani hauna madhara kwa jamii.
Alitaka wananchi kubeza wanaodai kuwa uchimbaji huo utakuwa na madhara kwani utafiti wa kutosha ulifanywa na kubaini kutokuwapo madhara yanayoweza kujitokeza.
Mkaguzi Mkuu wa Migodi wa Wizara ya Nishati na Madini, Edwin Konyani, alisema utafutaji urani ulianza mwaka 1980 ukishirikisha wataalamu kutoka Ujerumani.
Alisema Serikali imejiridhisha na utafiti uliofanywa na Wajerumani hao na wala haijakurupuka.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra kutoka Urusi, Asa Mwaipopo, alisema kampuni hiyo ndiyo itakayochimba urani katika mgodi huo na wanatarajia kuanza muda wowote baada ya kukamilisha taratibu.
Alisema kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa wa uchimbaji urani na imekuwa ikichimba sehemu kadhaa duniani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles