![]() |
Vishal Thakkar baada ya upasuaji (kushoto) na kabla. |
Mwanaume mmoja alizinduka baada ya upasuaji wa pua na kukuta daktari aliyemfanyia upasuaji huo kanyofoa pua yake yote.
Mgonjwa Vishal Thakkar alikwenda kwa Dk. Angelo Cuzalina, Rais wa Bodi ya Upasuaji wa Urembo Marekani, kwa ajili ya oparesheni zaidi ya nane katika kipindi cha zaidi miezi sita.
Thakkar alieleza kwamba baada ya kuwa ametengana na mkewe mwaka 2006, aliamua 'kufanya kitu fulani cha kibinafsi' na kufanyiwa upasuaji wa pua.
Japo kwa asili anatokea New York, Thakkar alikuwa akiishi huko Tulsa, Oklahoma wakati huo na kwenda kwa mmoja wa mabingwa wa upasuaji katika eneo hilo, Dk. Cuzalina.
Dk. Cuzalina hakuweza kupatikana kuzungumzia hili na wanasheria wake hapo awali walikataa maombi ya mahojiano na waandishi kwa madai kwamba hawawezi kuzungumzia kuhusu historia ya kitabibu ya Thakkar kwa kuzingatia makubaliano ya daktari na mgonjwa ni siri.
Thakkar anasema kwamba baada ya upasuaji wa kwanza alisumbuliwa na matatizo kidogo ya upumuaji ambayo humtokea wakati akilala au anapofanya kazi.
Alirejea kwa Dk. Cuzalina mara nane ndai ya mwaka huo mmoja kutibiwa hitilafu kadhaa kutokana na matibabu ya awali.
Kabla ya moja ya oparesheni hizo, Thakkari anadai kwamba alimweleza wazi mmoja wa manesi wa Dk. Cuzalina kwamba alikuwa hataki wachukue tishu yoyote kutoka kwenye masikio yake watakayohitaji kwa ajili ya pua yake wakati wa upasuaji huo.
Pale alipozinduka masaa kadhaa baadaye, alikuwa na maumivu nyuma ya masikio yake sababu walikuwa wamefanya hivyo. Inasemekana daktari huyo baadaye alimtumia Thakkar baruapepe kuomba radhi.
Tukio jingine linalofanana na hilo lilikuja pale walipoondoa tishu kutoka juu ya mbavu yake sababu waliishiwa tishu za kutosha kutoka kwenye sikio lake.
Kutapatapa kwa mwisho, hatahivyo, kulikuja pale alipozinduka kutoka kwenye oparesheni mwaka 2011 baada ya kupasuliwa ili kutibiwa maambukizi kadhaa.
Pale alipozinduka, hakuwa na pua.
"Alinieleza kwamba kulikuwa na maambukizi ndani yake na kwakuwa nilikuwa kwenye kitanda cha upasuaji na sikuwa na fahamu akalazimika kuchukua uamuzi huo," alieleza Thakkar.
Inaonesha kwamba uhusiano wa daktari na mgonjwa haukuwa mzuri kabla ya upasuaji huo unaotishia maisha, hatahivyo, hati ya mashitaka iliyofunguliwa na mwanasheria wa Thakkar inadai kwamba Dk. Cuzalina kwa siri alirekodi majadiliano yao kwenye ofisi za hospitali hiyo.
Hati hiyo ya mashitaka inasema Thakkar 'aliandikiwa kiasi kinachozidi cha dawa, kutosha kumuua mgonjwa huyo, kama angetumia, ikiwamo Loratab, Ambien, Valilum, na Oxycodone.'
Hii ni mbali na mwisho wa ndoto za upasuaji wa kurekebisha kiungo, hatahivyo, huku akitazamia kurekebisha sura yake.
"Hakuna jinsi nitaishi kama hivi. Ni mbaya zaidi ya kama ningekufa," alisema.