Jamaa mmoja kaokota pochi kwenye daladala. Alipofika kwake akapiga simu katika kituo kimoja cha redio na mambo yakawa hivi.
Jamaa: "Haloo, nimepiga simu kutangaza nimeokota pochi ndani ina Shilingi laki saba, kadi ya ATM, mkufu wa dhahabu na Blackberry tatu." Mtangazaji: "Asante sana. Sasa ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza?" Jamaa: "Hapana, ningependa kumchagulia wimbo wa R. Kelly unaoitwa YOU SAVED ME umfikie popote alipo!" Balaa...↧