![]() |
Rais Uhuru Kenyatta. |
Ushindi wa Uhuru Kenyatta katika kinyang’anyiro cha kihistoria cha Uchaguzi Mkuu wa Kenya, umeonesha kuwa siasa za ukabila nchini humo, bado zina nguvu.
Uhuru juzi alitangazwa kuwa Rais wa nne wa Kenya, baada ya kujipatia asilimia 50.07 ya kura zote zilizopigwa, dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, aliyepata asilimia 43.28 ya kura hizo.
Kwa mujibu wa Katiba mpya ya Kenya, mgombea wa urais, ni lazima afikishe zaidi ya asilimia 50 ya kura, masharti ambayo Uhuru aliyatimiza japo kwa asilimia 0.07.
Akizungumza jana, Mhadhiri wa Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, alisema siasa za ukabila ni saratani ambayo bado inaendeleao kuitafuna Kenya na kuwa jambo hilo si zuri kwa mustakabali wa nchi hiyo.
Alisema ukabila ni vigumu kuumaliza nchini humo, na imejionesha katika uchaguzi uliomalizika, jinsi wapigakura walivyokwenda kupiga kura zao kwa kumfuata mtu na si sera na itikadi za vyama.
Kauli hiyo pia imeungwa mkono na mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Audax Kweyamba, aliyesema kuwa Kenya bado inasumbuliwa na donda la ukabila.
“Nimefuatilia sana uchaguzi wa Kenya, hata ushindi unaonesha kabisa siasa za ukabila ni tatizo jambo ambalo si zuri kwa mustakabali wa nchi hiyo,” alisema.
Bana alisema katika kutekeleza kauli yake ya kuunda Kenya moja, ni vema Uhuru aje Tanzania kujifunza msingi ya kujenga taifa kama alivyofanya Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere.
“Uhuru kama anataka kujenga nchi yenye umoja, aje kujifunza namna ya kujenga taifa, lakini hili hawezi kumaliza peke yake, isipokuwa kwa kusaidiwa na kambi ya Odinga na Wakenya kwa ujumla.
“Kinyume chake Wakikuyu (kabila la Uhuru) na Wakalenjini (kabila la Mgombea Mwenza, William Ruto), wataendelea kuongoza kwa sababu ndio wengi na wanajitokeza kupiga kura,” alisema Dk Bana.
Kweyamba yeye alishauri Uhuru ateue viongozi au mawaziri, kulingana na uwezo wao na kuzingatia sura ya utaifa ili kuondoa picha ya ukabila iliyojengeka.
Akizungumzia ushindi mwembamba wa Uhuru, Dk Bana alisema haijalishi, ilimradi Katiba ya Kenya iliyopitishwa na wananchi wenyewe, inaruhusu mshindi kutangazwa akiwa amefikia zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Hata hivyo, alisema ni vema nchi za Afrika ikiwemo Tanzania inayojiandaa kupata Katiba mpya, ziangalie suala hilo katika katiba zao.
Alipendekeza Katiba ziagize uundwaji wa Serikali ya Umoja ya Kitaifa, endapo kunakuwa na kuzidiana kwa kura chache, ili kuondoa manung'uniko kwa walioshindwa.
“Katika hali ya kawaida, ukishindwa kwa tofauti ndogo huamini matokeo, lakini hili linaweza kumalizwa kwa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kinyume chake kiongozi aliyeshinda, atatawala kwa nguvu ya dola kutokana na sehemu kubwa kumpinga,” alisema.
Naye Kweyamba alisema jambo la msingi ni hiyo asilimia 0.07 iliyompa Uhuru ushindi, iwe imetokana na Tume kuendesha uchaguzi huru na wa haki na imepatikana kihalali.
Kweyamba alisema Kenya imevunja rekodi ya idadi kubwa ya wapiga kura kujitokeza kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi, kwa kile kinachoonekana ni kuwa na matumaini mapya baada ya vurugu zilizotokea mwaka 2007.
“Tuombe Mungu, mambo yote yaishe salama na Kenya iwe salama, kwani endapo kutatokea machafuko, kuna hatari ya kushusha morali ya wananchi, ambao wamejitoa kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi,” alisema Kweyamba.
Alisema, Watanzania wanatakiwa kujifunza namna ya kutumia haki ya kuchagua vongozi, na kuachana na tabia ya kuona kuwa hawana haja ya kushiriki kwenye uchaguzi. Alisema asilimia 42.8 zilizofikiwa mwaka 2010 haikuwa idadi nzuri.
Naye Dk Bana alisema hiyo ni hatua nzuri, ambayo inaonekana imechangiwa na vyama siasa vya Kenya kutoa hamasa kwa wananchi na jinsi Serikali ilivyofanya kazi ya kutoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi wake.