![]() |
Absalom Kibanda akiwa hospitalini. |
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (Tef), Absalom Kibanda, ameanza kupata nafuu baada ya upasuaji wa saa 05.30 uliofanyika juzi.
Taarifa ya Katibu wa TEF, Neville Meena, kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa kulipopambazuka jana, Kibanda aliamka akiwa na nafuu, kuliko ilivyokuwa siku za kwanza.
“Sura yake imeanza kurejea katika hali ya kawaida, uvimbe wa damu zilizokuwa zimevilia ndani zimepungua. Hata kuzungumza kwake kuliwatia matumaini wanaomuuguza,” alisema Meena katika taarifa hiyo.
Operesheni aliyofanyiwa Kibanda kwa mujibu wa Meena, ni pamoja na ya kuondoa jicho la kushoto na kurekebisha taya ya kushoto. Taya hiyo na meno ambayo yalibainika kupata mtikisiko, vimefungwa kwa waya maalumu, ili virejee katika hali ya kawaida.
Kuhusu jicho lililong’olewa, Meena alisema madaktari wameahidi kuweka jicho la bandia ambalo hata hivyo halitamwezesha kuona. Jicho hilo linasubiri uamuzi wa madaktari hao ambao wanasubiri apone jeraha alilopata.
Upasuaji huo pia umeelezwa kwamba ni wa kitaalamu na haukuhusisha upasuaji wa kutumia kisu, bali ni wa kutumia matundu ya pua na kutatua matatizo yaliyokuwa yakimkabili kwa ndani. Kwa maana nyingine hakuna majeraha yoyote yaliyotokana na upasuaji huo.
"Kwa sasa Kibanda anaendelea na matumizi ya dawa, chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Millpark, Johannesburg.
Kama ambavyo tumekuwa tukihimizana, hiki ni kipindi kigumu katika tasnia yetu ya habari kwa ujumla. Nachukua fursa hii kuwaomba kwamba tuendelee kumwombea Mwenyekiti wetu ili Mungu aweze kumponya mapema," alisema Meena katika taarifa yake.