Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

POLISI WAUA DEREVA TAKSI KWA KUMFUNGA NA KUMKOKOTA KWENYE GARI MITAANI...

Image may be NSFW.
Clik here to view.
KUSHOTO: Mido Macia akikokotwa kwenye gari la polisi mitaani. KULIA: Mido akiwa na dada yake kabla ya mkasa huo.
Maofisa wanane wa polisi wanaotuhumiwa kumfunga pingu dereva taksi Mido Macia kwenye gari lao la doria na kumkokota mitaani hadi alipofariki, wamekamatwa kwa kesi ya mauaji.
Picha za video zilizonaswa kwenye simu ya mkononi zimeonesha maofisa hao wakiwa wamemfunga raia huyo wa Msumbiji mwenye miaka 27 nyuma ya gari lao na kukimbiza gari hilo kwa kasi mbele ya umati uliojawa hofu uliokuwa ukishuhudia.
Mido alikutwa amekufa kwenye selo ya polisi masaa mawili baadaye huko Daveyton, Afrika Kusini.
Mkuu wa Polisi nchini humo jana alisema 'amepatwa na mshituko mkubwa' kutokana na video hiyo, huku akitangaza maofisa waliohusika wamesimamishwa na kamanda wa polisi wa eneo hilo ameondolewa katika cheo chake.
Jenerali Riah Phiyega alisema anashirikiana kwa nguvu zote katika uchunguzi huo na wakala wa wapelelezi wa polisi na kuongeza haki za Mido 'zilivunjwa kwa kiwango kikubwa mno.'
Wachunguzi walisemekana kuelezwa kwamba dereva taksi huyo alimshambulia mmoja wa maofisa hao wa polisi na kuchukua bunduki yake.
Lakini gazeti la Daily Sun la nchini humo jana lilibainisha kwamba picha mpya za video zinazoonekana kujichanganya mlolongo wa matukio yaliyoelezwa na maofisa.
Inaonekana kuonesha dereva taksi huyo akizozana na maofisa wa polisi huku akitupa mikono yake, kabla ya kudhibitiwa chini na zaidi ya wanaume watano waliovalia sare.
Sakata hilo ni jipya kabisa kushusha kujiamini kwa polisi Afrika Kusini, likiibua rundo la aibu nyingine zaidi kwa vikosi vilivyowamiminia risasi wafanyakazi waliokuwa wakiandamana katika mgodi wa Marikana mnamo Agosti mwaka jana na kuua watu 34.
Pia limekuja huku kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius ikiuweka mfumo wa sheria wa nchi hiyo katika njiapanda.
Mido alikamatwa kwenye mji wa Daveyton nje ya Johannesburg Jumanne jioni. Shuhuda ambaye hakutaka kujitambulisha alilieleza gazeti la mjini humo: "[Polisi] walizozana na Mido na kisha wakampiga.
"Walimfunga pingu nyuma ya gari lao na kumbamiza usoni na mlango.
"Huku damu ikichuruzika usoni mwake waliondoa gari hilo kwa kasi. Alikuwa katika maumivu makali. Alilia na kuwaomba askari hao wasimamishe gari lakini hatahivyo waliendelea na safari."
Kurugenzi ya Polisi ya Uchunguzi Binafsi Afrika Kusini, ambayo imeanzisha uchunguzi, ilisema inawezekana sababu za kifo kilikuwa majeraha kichwani na kuvilia kwa damu mwilini.
Msemaji wa Kurugenzi hiyo, Moses Dlamini alisema wachunguzi walielezwa Mido alitakiwa kuondosha taksi yake na polisi wawili sababu ilikuwa imeziba barabara.
Kisha Mido anadaiwa kumshambulia mmoja wa maofisa na kuchukua bunduki yake, kabla maofisa kufanikiwa kumdhibiti na kumpakia kwenye gari lao kumpeleka selo.
Mfungwa mmoja aliyekuwa kwenye kituo cha polisi alisema: "Walimuua. Walimpiga vibaya sana humu ndani."

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles