Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

SARATANI YAPOKA UHAI WA MWIGIZAJI WA "ONE DAY AT A TIME"...

$
0
0
Bonnie Franklin.
Bonnie Franklin -- ambaye alikuwa nyota akicheza kama Ann Romano katika Kipindi cha Televisheni cha "One Day at a Time" -- amefariki dunia jana kufuatia matatizo ya saratani ya kongosho akiwa na umri wa miaka 69.
Franklin alitangazwa kugundulika na saratani ya kongosho mnamo Septemba mwaka 2012.
Bonnie alifanya kazi kwa kipindi kirefu, lakini alifahamika zaidi alipocheza kama mama wa Valerie Bertinelli na Mackenzie Phillips kwenye "One Day at a Time" kuanzia mwaka 1975-1984.
Aliolewa na Ronald Rossi kuanzia mwaka 1967 hadi 1970 na kisha akaolewa tena na prodyuza Marvin Minoff kuanzia mwaka 1980 hadi alipofariki prodyuza huyo Novemba 2009. Hakubahatika kupata watoto.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles