Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

RUBANI ABADILI UELEKEO WA NDEGE SABABU YA 'GIZA TOTORO' UWANJA WA NDEGE...

$
0
0
Kisiwa ambacho ndege hiyo ilikuwa itue hapo.
Ndege ya Ryanair ilibadili uelekeo maili 200 kufikia uwanja mwingine wa ndege mbali na kituo cha mwisho wa safari yake kwenye kisiwa cha mapumziko nchini Ugiriki sababu rubani wake alisema 'kulikuwa na giza nene kuweza kutua'.

Abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo kutoka uwanja wa Stansted, London kwenda Kefalonia walijawa na hasira pale walipokuwa wameelezwa ndege yao inatakiwa kubadili uelekeo.
Waliishia kwenye Uwanja wa Ndege wa Thessaloniki ulioko Ugiriki bara majira ya usiku sababu ya matatizo hayo.
Watu waliokuwamo ndani yake mwanzoni walidhani ndege hiyo ilikuwa imeishiwa mafuta hadi rubani huyo alipotoa tangazo lake.
Mara waliweza kuruka tena na kupaa kuelekea kwenye kituo cha mwisho cha safari yao baada ya kuchelewa kwa masaa mawili.
Abiria na mwandishi wa habari Kate Mansey, ambaye alikuwamo kwenye ndege hiyo, alituma jumbe kwenye mtandao wa Twitter: "Katika ndege ya Ryanair ambayo imetua katika kisiwa kisicho cha Ugiriki. Kisingizio? "Giza mno" kuweza kutua katika uwanja wa ndege sahihi. Abiria wenye gadhabu."
Alidai ndege zilikuwa zikiruhusiwa tu kutua kwenye uwanja huo wakati wa 'saa za mchana' - japo ndege hiyo ilipangwa kutua majira ya Saa 3:20 usiku.
Hatimaye pale waliporuhusiwa kusafiri kwenda kituo cha mwisho wa safari yao usiku mnene abiria mmoja akauliza 'jua limetokeza katika Keffalonia mwishowe?"
Mansey aliongeza baadaye: "Kwa sasa tunaruka tena kuelekea kituo chetu cha awali cha Keffalonia. Pengine wamepata tochi. Safi sana."
Msemaji wa Ryanair alikosoa 'masharti ya kutua/kuruka' kwamba yalisababisha uchelewaji huo.
"Ndege ya Ryanair namba FR6611 kutoka Stansted kwenda Kefalonia mnamo Mei 13 ilibadili uelekeo na kwenda Thessaloniki kufuatia masharti ya kutua ambayo yanakataza ndege za usiku za Ryanair kutua Kefalonia.
"Ndege hiyo ilitua kawaida kwenye uwanja wa Thessaloniki na kuelekezwa kwenda Kefalonia (masaa mawili baadaye) mara baada ya kizuizi hiki kuondolewa. Ryanair inaomba radhi kwa abiria walioathirika na kuchelewa huku kwa masaa mawili.
"Ryanair imerekebisha ratiba hizo za muda kwa ndege zake zinazoenda Kefalonia kuhakikisha kwamba kizuizi cha mida ya kutua usiku hakileti athari."
Safari hizo za ndege za gharama nafuu mara mbili kwa wiki kwenda Kefalonia zilizinduliwa Aprili 1, mwaka huu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles