![]() |
KUSHOTO: Chumba cha nyumba ya kulala wageni mjini Oxford ambacho kilitumika kwa unyama huo. JUU: Mohammed Karrar. CHINI: Bassam Karrar. |
Mateso kwa mmoja wa waathirika yalianza baada ya kuhaha kwa udi na uvumba kupata mpenzi yeyote na uangalizi wa karibu sababu alikuwa amelazimishwa kuwatunza wazazi wake ambao ni wagonjwa.
Hivyo pale Mohammed Karrar alipoingia maishani mwake, akimnunulia uturi na kumchukulia kama mtu mzima, alimwamini. Lakini 'kipindi cha fungate la kuvutia,' kama alivyolielezea, lilidumu ndani ya mwaka mmoja.
Baada ya kumfanyia mambo ya kikubwa, Karrar alihakikisha 'anamsahaulisha' kwa kumywesha pombe na dawa za kulevya kabla ya kumbaka kwenye sofa.
Kuanzia hapo binti huyo akawa 'mali' yake na mtumwa wa ngono aliyemkodisha kwa wadhalilishaji kote nchini humo kwa dau la hadi Pauni za Uingereza 600 kwa saa.
Zaidi ya miaka mitano alishambuliwa kwa kurudia-rudia katika kile alichoelezea kama 'ngono ya maumivu'. Huku akichomwa sindano za dawa za kulevya aina ya heroin, aliuzwa kwa makundi ya wanaume wa Kiasia ambao walimbaka kwa wote kwa pamoja katika viti vya kando ya kitanda na nyumba za kulala wageni zilizoko mjini Oxford na kwingineko.
Sasa akiwa na miaka 19, muathirika huyo aliyetambulishwa kama Girl D kwa sababu za kisheria, mara kwa mara alitokwa machozi wakati akitoa ushahidi kupitia video huku akielezea mateso yake ya kutisha.
Kufuatia ubakaji huo, mashambulio ya kinyama ya Karrar yalikuja kuwa mazoea na wakati mwingine alitengeneza filamu za 'ngono' kwa kumtumia msichana huyo.
Kama akikataa, alimpiga na kumtishia kwa silaha, wakati fulani akimpiga kwa kutumia gongo la kuchezea mpira wa base.
Alifikia hata kumbaka msichana huyo, ambaye ametokea kwenye familia yenye matatizo, kwenye nyumba hiyo aliyokuwa akichangia na wazazi wa msichana huyo.
Karrar na kaka yake Bassam, ambaye hakupatikana na hatia sambamba na wanaume wengine watano kwenye mlolongo wa mashitaka ya ubakaji, alimlazimisha binti huyo kufanya ngono na mmoja wao wakati akiendelea kufanya mapenzi na mwingine.
Kwa huzuni huku akikumbukia kumweleza Karrar kuhusu ujauzito wake, binti huyo alisema: "Alifura kwa hasira. Alisema nilitakiwa kuwajibika kwa kiasi fulani."
Alipatiwa vidonge viwili, akapelekwa kwenye nyumba moja mjini Reading ambako alilazimishwa kufanyiwa utoaji mimba kinyume cha sheria kwa kutumia ndoana ndefu.
Msichana huyo alisema hawezi kukumbuka zaidi kuhusu mchakato huo, lakini anaamini ulifanyika kwenye sakafu ngumu ya sebule. Hakukuwa na madaktari wala manesi, hakukuwa na dawa za kutuliza maumivu au tiba.
Wakati fulani, Karrar alimbandika alama kwa kutumia chuma cha moto kwenye nyama yake.
"Alikuwa akinibandika alama ili kwamba kama nitafanya ngono na yeyote mwingine, watu wangejua kwamba nilikuwa wake," alisema.
Zaidi ya miaka minne iliyofuatia Karrar alimtembeza msichana huyo nchi nzima na kumuuza kwa 'Pauni 600 kwa mara moja'.
Alivalishwa sketi fupi na vizibao vifupi kabla ya kubakwa kwa kurudia-rudia. Sherehe zilifanyika ambapo alitakiwa kukidhi matakwa ya kimapenzi na hadi kufikia 'wageni muhimu' 15.
Baadaye alihamishiwa kwenye familia ya kufikia mbali na Oxford na ndoto hiyo ikakoma.
Miaka miwili baadaye alikutana na Karrar baada ya mwanaume huyo kuwa amemshawishi kwamba amebadilika kitabia.
Wakati wa majadiliano nyumbani kwake binti huyo alitaka kujua kwanini alimdhalilisha na kumuuza kwa ajili ya ngono. Karrar alipandwa na hasira na kumbaka binti huyo kwa mara ya mwisho.
Mmoja wa waathirika alisema alikuwa amepumbazwa na wadhalilishaji wake ambao hadi sasa wakati mwingine kushindwa kuona ufedhuli wa wanaume hao ambao walimbaka.
Akifahamika tu kama 'Girl Three', alipitia miaka mitatu ya udhalilishaji kwenye mikono ya genge hilo.
"Ilikuwa ni kupumbazwa. Hata kwa siku hii naweza kusema kabisa, 'Hawakuwa na tatizo'," alisema.
"Walinifitinisha na mama yangu. Walifahamu kila kitu ambacho walitaka kumwambia mtu aliye kwenye hatari, mtu wa rika dogo, kwa upande wao."
Kama ilivyo kwa waathirika wengi, alipitia udhalilishaji kama mtoto na alikuwa katika uangalizi.
Baadaye aliasiliwa lakini aliasi kwa kutorokea mbali na kulewa pombe.