![]() |
KUSHOTO: Ufukwe wa South Carolina. JUU: Kyle Martin Schnoebelen. CHINI: Jasmine Kim Walton. |
Wapenzi wamekamatwa katika ufukwe wa South Carolina baada ya polisi kuwabamba wakiwa hawajavaa nguo na mmojawao 'akiwa amelewa kupindukia'.
Jasmine Kim Walton, miaka 21, na Kyle Martin Schnoebelen, miaka 22, wote kutoka Virginia walikamatwa muda mfupi kabla ya kufikia Saa 9 alfajiri ya Jumapili.
Waliwaeleza polisi kwamba walikuwa wamekwenda kuogelea kwa kupiga mbizi na waliporejea wakakuta nguo zao zimeibwa.
Walton ameshitakiwa kwa uvukiukaji wa maadili hadharani na kukaa uchi baada ya kuwa ameshindwa kutoa ushirikiano na kuwa mbishi wakati alipofuatwa na polisi.
Ripoti hiyo ilisema lugha yake haikuwa ya kiungwana, alikuwa akinuka pombe na kukaidi kuwapa maofisa hao wa polisi jina lake au anwani.
Schnoebelen alishitakiwa kwa kukaa uchi hadharani.