Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

POLISI 16 WAINGIA MATATANI KWA TUHUMA ZA KUSHIRIKI MAGENDO...

$
0
0
Kamanda Suleiman Kova.
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inawashikilia askari wake 16 wa vyeo mbalimbali, kwa tuhuma za kushiriki na kuendekeza mtandao wa wafanyabiashara wa magendo.

Magendo hayo yanadaiwa kuvushwa kupitia bandari bubu zisizo rasmi maeneo ya Kawe hadi Bagamoyo, kwa msaada wa askari hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema wataalamu wa intelijensia kupitia teknolojia ya kisasa, walibaini askari hao kwa nyakati mbalimbali wakishirikiana na wafanyabiashara hao, wakiwapa hongo  ili wasichukuliwe hatua za kisheria.
“Hadi sasa askari tuliowakamata ni 16 wa vyeo mbalimbali na wapo chini ya ulinzi, wakiendelea kuhojiwa. Majina yao tunayahifadhi kwa sasa kwani bado wapo wengine tunawatafuta ili kubaini mtandao mzima na kusafisha jeshi letu,” alisema.
Alisema pamoja na jeshi kuwa na askari waliofanya vizuri, hadi kupewa vyeti na nishani kwa utendaji mzuri na wa kuigwa, lakini bado kunakuwepo na wachache ambao vitendo vyao vinavyokiuka maadili ya Polisi.
“Baada ya kupata taarifa kwa raia wema, tumeshirikiana na wananchi na kufuatilia nyendo za askari wachache, ambapo taarifa zilieleza walikuwa wakiendekeza mtandao wa wafanyabiashara wa magendo, ambao huvusha mali kupitia bandari bubu,” alisema.
Alisema askari hao pia wanatuhumiwa kushiriki na kutochukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanaofanya magendo, na badala yake wameonekana wakiwafuatilia na baadaye kuelewana na kupewa rushwa.
Alisema operesheni hiyo pia imewalenga wafanyabiashara pamoja na wafanyakazi wa taasisi na idara zote za Serikali, ambazo zitabainika kuhusika   kufanya magendo hayo.
Kova alisema jeshi hilo halitavumilia kikundi chochote  kitakachowaharibia muonekano wa jeshi hilo, kwa kuwa lengo lao ni kuunda jeshi safi, la kisasa na lenye weledi.
“Tunawashukuru wananchi kwa jitihada za kushirikiana na polisi kubaini maovu katika Jeshi kwa lengo la kusafisha maovu, utaratibu huu ni endelevu na ni fundisho kwa yeyote atakayejaribu kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi,” alisema.
Hata hivyo alisema uchunguzi zaidi unafanyika, na kwa yeyote atakayebainika kufanya kosa lolote la jinai watachukuliwa hatua na wale watakaoonekana hawana hatia, wataachiwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

Trending Articles