Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

ALIYEZINDUKA BAADA YA AJALI NA KUJIGUNDUA MJAMZITO, AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME...

$
0
0
Gemma akiwa amembeba mtoto wake, Ruben.
Mwanamke mmoja ambaye alizinduka baada ya kuzirai na kugundua ana ujauzito wa wiki nne amesimulia furaha yake baada ya kujifungua mtoto 'kamilifu' wa kiume.

Madaktari waligundua muathirika wa ajali ya gari Gemma Holmes, miaka 26, alikuwa mjamzito wa wiki nne pale alipofikishwa hospitalini baada ya kugongana na gari lililoegeshwa wakati akiendesha gari Septemba, mwaka jana.
Gemma - ambaye amekuwa akitembelea kiti cha magurudumu tangu apate ajali hiyo sababu ujauzito wake ulimzuia kufanyiwa upasuaji kuokoa maisha -  alipatiwa taarifa za kushangaza pale alipozinduka takribani miezi mitatu baadaye.
Miezi mitano mbele, Gemma, kutoka Dilton Marsh, Witshire, akajifungua mtoto wa kiume, Ruben.
"Sikuweza kujizuia kulia pale kwanza nilipooneshwa, sababu ni mtoto wangu wa muujiza mdogo," alisema.
"Nilikuwa na furaha mno kumuona baada ya kila kitu tulichopitia."
Sio tu kwamba Gemma hakuwa na taarifa kwamba anatarajia kujifungua pale alipozinduka, usahaulifu aliokuwa nao kufuatia ajali hiyo ulimaanisha miaka hiyo mitatu iliyopelekea hali hiyo ilifutika katika kumbukumbu zake.
Kuongezea kwenye mkasa wake, mama huyo mpya amekuwa kwenye kiti cha wagonjwa tangu ajali hiyo sababu madaktari walimwepusha kufanyiwa upasuaji wa kuokoa maisha wa mgongo wake kufuatia kugundulika kuwa nu mjamzito.
Lakini sasa Ruben amewasili kwa madaktari wamemweleza mama huyo mwenye miaka 26 kwamba atajifunza tena kutembea, huku upasuaji wake ukipangwa kufanyika katika kipindi cha miezi sita.
"Madaktari wamesema watanifanyia upasuaji wa mgongo wangu baada ya Ruben kufikisha miezi sita, sababu nanyonyesha na wanataka kunipatia muda wa kutosha," alisema Gemma.
"Madaktari watalazimika kupasua mgongo wangu tena na kupachika vyuma ndani. Kisha hapo nitakuwa na miaka mingine miwili ya kutembea kwa kutumia kiti kabla hawajafikiria kuweza kutembea na kukimbia na mwanangu."
Gemma alipata majeraha makubwa kichwani na shingoni katika ajali mbaya ya gari mnamo Septemba mwaka jana na alisafirishwa kwa ndege hadi hospitalini akiwa hajitambui.
Hatimaye akazinduka kwa mara ya kwanza Oktoba baada ya kurejeshwa tena katika hali hiyo hadi Desemba.
Ruben alizaliwa Alhamisi katika Hospitali ya Royal United iliyoko mjini Bath na amekuwa chini ya uangalizi wa mama yake na bibi yake, Julie Brown.
Gemma, ambaye alitengana na mumewe, Dicks, mwenye miaka 31, wiki mbili kabla ya ajali yake, alisema: "Manesi katika hospitali hiyo walikuwa mahiri sana, ambao walinisaidia kuniweka katika hali nzuri.
"Mama yangu amekuwa wa aina yake na ananisaidia mno, lakini naweza kumnyonyesha na pia nilimbadili nepi kwa mara ya kwanza jana."
Wakati Gemma akisema hawezi kurudiana na baba wa Ruben, Dicks amekuwa akiwatembelea wote mama na mtoto.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles