Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

KESI YA AKINA MRAMBA KUSIKILIZWA SEPTEMBA 9

$
0
0
Kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake, inatarajia kuendelea kusikilizwa Septemba 9 hadi 12 mwaka huu.
Hakimu Mkazi, Frank Moshi alisema hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Mbali na Mramba, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Mipango na Uchumi, Gray Mgonja.
Katika kesi hiyo, washitakiwa wote wanadaiwa kuwa kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Ilidaiwa kuwa walisababisha hasara hiyo baada ya kutoa msamaha wa kodi kinyume cha sheria kwa Kampuni ya M/S Alex Stewart ya nchini Uingereza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles