Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4561

KAMATI KUU CHADEMA YAKUTANA LEO

$
0
0
Kamati Kuu ya Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inakutana leo jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho cha kawaida ni cha siku mbili na pamoja na mambo mengine kitakajadili masuala ya mchakato wa Katiba mpya na rufaa zilizokatwa na wanachama wake.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na chama hicho, ilieleza kuwa katika siku hizo mbili, pia wajumbe watapokea na kujadili taarifa ya hali ya siasa nchini; uchaguzi wa ndani ya chama na taarifa ya fedha, mpangokazi na bajeti.
Aidha pia, wajumbe watajadili mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, kanuni na miongozo ya mabaraza ya chama hicho, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4561

Trending Articles