Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

WASTAAFU TAZARA WALALMIKIA MALIPO KIDUCHU

$
0
0
Wastaafu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wamelalamikia uongozi wa shirika hilo kwa kulipa malipo yao kwa kufuata utaratibu ambao hautambuliwi na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Tazara jana walipokusanyika wastaafu hao, Katibu wa wastaafu, Ayasi Mbonde alisema malipo yao yaliyoidhinishwa Sh bilioni 12 kutokana na uchunguzi uliofanywa na ofisi ya CAG na walitarajia ulipaji ufuate viwango vilivyoainishwa na CAG katika ripoti yake.
Alisema kwa kutoridhikwa wao waliamua kwenda Wizara ya Uchukuzi kulalamika ambapo walikaa kikao na Mkurugenzi wa usafirishaji na baadaye kuomba kufanyika kikao kati ya wastaafu hao, CAG na uongozi wa Tazara kujua tatizo liko wapi lakini hata hivyo kikao hicho hakijafanyika mpaka sasa .
Meneja Mkuu wa Tazara wa mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Shekimweri alisema ni kweli kuna kikao ambacho kilitakiwa kuwepo kati ya uongozi wa Tazara, CAG na uongozi wa wastaafu hao lakini kwa bahati mbaya tarehe zilizopangwa uongozi wa Tazara nao ulikuwa na vikao vyao vya juu ikiwa ni pamoja na vikao vya bodi.
“Tarehe alizotupangia CAG na sisi tulikuwa na vikao lakini hata hivyo tunaendelea kufanya mawasiliano nao kupata siku ambayo tutakutana,” alisema Shekimweri ambaye alikataa kuzungumzia madai ya wastaafu hao mpaka pale yatakatolewa maelekezo katika kikao na CAG.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

Trending Articles