Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4558

WAFANYAKAZI WA VODACOM WAPEWA 'KINGA' YA AJALI

$
0
0
Kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua kampeni maalumu ya kuhamasisha wafanyakazi wake kuhakikisha uendeshaji wa magari na vyombo vingine vya moto ili kulinda afya na usalama wao wawapo barabarani.
Vodacom ambao ni washindi wa tuzo ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi inayotambuliwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (Osha) imezindua kampeni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zake kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake wanapokuwa kazini.
Kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Wait to Send’  inawataka wafanyakazi wa Vodacom wanaotumia magari ya kampuni na wasiotumia kutotumia simu ya mkononi kutuma ama kusoma ujumbe mfupi wa maandishi ili kujiweka katika mazingira salama ya kujikinga na ajali wawapo barabarani.
“Tunayo furaha kubwa sana leo kuona tunapiga hatua nyingine moja ya ziada katika kulinda afya na usalama wa wafanyakazi wetu wakati wote.
Hili ni jukumu letu tunalolipa kipaumbele cha hali ya juu katika uendeshaji wa shughuli zetu,” alisema Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare.
Alisisitiza: “Kila mfanyakazi wetu lazima awe salama na tunapotambua uendeshaji wa majukumu yetu ambayo matumizi ya magari na vyombo vingine vya usafiri ni sehemu ya kazi zetu, ni lazima tukumbushane njia bora za uendeshaji ulio salama kwa faida yao na kwa kampuni pia.”
Lwakatare alisema ingawa hakuna ajali nyingi zinazohusisha wafanyakazi wakiwemo wakandarasi wake, hali hiyo haiwezi kuifanya Vodacom kujisahau kwani lengo ni kuhakikisha hata hizo chache zinazojitokeza zinadhibitiwa na kuepukwa.
Alisema matumizi ya simu za mkononi kwa madereva ni moja ya visababishi vya ajali na hasa kutumia simu ya mkononi kutuma au kusoma ujumbe mfupi wa maadishi.
Kampuni inataka kila mfanyakazi kutambua hilo na kujikinga dhidi ya janga analoweza kupata kwa kutumia simu yake anapoendesha gari.
Alisema Vodacom inaangalia namna gani wanaweza kushirikiana na Polisi na wadau wengine kuhusisha jamii nzima na kampeni hiyo kupunguza ajali za barabarani zinazochangiwa na matumizi ya simu za mkononi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4558

Trending Articles