Wakazi watatu wa Dar es Salaam jana walikamatwa na polisi kwa tuhuma ya kujiunganishia maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) kinyume cha sheria.
Walikamatwa mbele ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na viongozi wa Dawasa na Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco).
Watu hao walikamatwa Ubungo-Maji na Kimara Temboni katika Manispaa ya Kinondoni kwa nyakati tofauti. Watu hao walikutwa wakiwa na wafanyakazi kadhaa, wakifyatua matofali.
Katika eneo la Kimara Temboni, bomba kubwa la Dawasa lilikutwa limetobolewa kisha bomba dogo limeunganishwa kwenye bomba hilo kubwa. Bomba hilo dogo linamwaga maji usiku na mchana na ndilo linalotoa maji, yanayotumika kufyatua lundo la matofali.
Katika eneo la Ubungo Maji, umbali wa mita chache kutoka ofisi za Wizara ya Maji, wahusika walidai maji wanayotumia kufyatulia tofali, yanatoka mtoni, wakati si kweli.
Makalla alisema kukamatwa kwa watu hao, kunatokana na ripoti ya Kamati Maalum iliyoundwa na wizara hiyo, kufuatilia upotevu wa maji yanayozalishwa na Dawasa.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa maji mengi yanapotea Jijini humo, kutokana na wizi wa maji, unaofanywa na watu wachache, wakiwemo wafyatua matofali.
Alisema kuna watu 40 wamebainika hadi sasa kuwa ni wezi wa maji ya Dawasa na kwamba wote hao, watakamatwa na vyombo vya dola katika operesheni kali inayoendelea.
Katika ziara hiyo ya kukagua miradi ya Dawasa, Makalla alitembelea matangi makubwa ya Dawasa yaliyopo Chuo Kikuu cha Ardhi na kuagiza mamlaka hiyo, kuharakisha ukarabati wa matangi hayo. Baadaye, alitembelea mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu.
Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Va Tech Wabag ya India. Ulianza Februari mwaka huu na utakamilika Agosti mwakani. Tayari mkandarasi huyo ameanza kazi ya ujenzi wa chujio mpya ya mtambo huo wa Ruvu Juu.
Alipotembelea matangi ya Chuo Kikuu cha Ardhi, alikuwepo pia Mbunge wa Kawe, Halima Mdee(Chadema). Alipokagua mradi wa upanuzi wa Ruvu Juu, alikuwepo pia Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamud Abuu Jumaa (CCM).