Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4558

MCHUNGAJI MSIGWA ATAKA KAMPUNI ZA UWINDAJI ZICHUNGUZWE

$
0
0
Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, ametaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya kampuni zote za uwindaji,  kubaini matukio ya ukiukwaji wa sheria za wanyamapori,  unaosababisha taifa kupata sifa mbaya.
Aidha, ametaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwawajibisha baadhi ya watendaji wote wa wizara hiyo kwa kushindwa kutekeleza ipasavyo wajibu na majukumu yao katika kusimamia sekta ya wanyamapori, hivyo kusababisha ukiukwaji wa sheria katika uwindaji.
Alisema hayo Jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya matukio ya ukiukwaji wa sheria za uwindaji katika hifadhi ya Selous.
Msigwa, ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini alisema kuna ushahidi wa uwepo wa matukio ya  kijangili, yaliyofanywa na kampuni moja na serikali inapaswa kuchukua hatua.
 “Naiomba Serikali kuzifanyia uchunguzi kampuni zote za uwindaji nchini. Pamoja na hilo, Wizara ya Maliasili itoe adhabu kali kwa kampuni zote za uwindaji ambazo zitachunguzwa na kukutwa na hatia katika  makosa yote uwindaji haramu ili iwe fundisho kwa kampuni na watu wengine wote wanaovunja kwa makusudi sheria na kanuni zilizowekwa,” alisema.
Miongoni mwa matukio ambayo, Waziri huyo kivuli alionesha video kwa waandishi wa habari, akilalamikia uwindaji wa wanyama waliokatazwa kwa mujibu wa sheria na matumizi ya silaha zisizotoa milio kinyume na Kifungu Namba 64 (2),  chenye zuio la silaha zisizoruhusiwa kutumika katika uwindaji.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4558