Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

NCCR-MAGEUZI YAMKINGIA KIFUA KAFULILA

$
0
0
Kitengo cha Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema kinamuunga mkono mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama hicho, David Kafulila, kuhusu harakati za kutaka uchunguzi huru kuhusu suala la fedha za akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu (BoT) inayoihusu kampuni ya  IPTL.
Kwa sasa tangu kuibuka kwa suala hilo, uongozi wa Bunge ambao Kambi Rasmi ya Upinzani ni sehemu yake, uliridhia Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya uchunguzi na kupeleka taarifa yake bungeni.
Pamoja na taasisi hizo ikiwemo ya CAG ambayo inaaminika kimataifa kukabidhiwa suala hilo, bado Kafulila na Kitengo cha Vijana wa NCCR, wameamua kufanya ziara nchi nzima, kutoa wanachokiita ni elimu  kwa Watanzania juu ya suala hilo, huku kaulimbiu ikiwa ‘Rejesha Fedha Zetu’.
“Kwa matusi yalitotolewa hadi sasa kuhusu sakata hili na baadhi ya viongozi wa nchi hii, yanatosha kuwa aibu kubwa kwa taifa, lakini sisi hatuogopi kuitwa tumbili, tutaendelea kusimamia suala hili hadi fedha hizi zirejeshwe,” alisisitiza Meck.
Alisema ziara yao ya nchi nzima, wanatarajia kuianza wiki ijayo na wataanza na mkoa wa Kigoma, ambako wananchi wataelimishwa juu ya sakata hilo huku hoja yao kubwa ikiwa ni kutaka kurejeshwa kwa fedha hizo.
Aidha, Meck aliwataka Mwanasheria Mkuu, Frederick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kueleza bayana nini kinachoendelea kuhusu suala hilo, na siyo kutoa vitisho.
“Kitendo cha Kafulila kuitwa tumbili pamoja na kumdhalilisha, kimelidhalilisha pia Bunge na wabunge lakini pia kimewadhalilisha wananchi wa Kigoma Kusini, kwa kuwa sasa wanaonekana wamemchagua tumbili kuwaongoza,” alidai.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles