Kampuni ya Bia Tanzania TBL imekabidhi hundi ya Sh milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa kisima kikubwa cha majisafi na salama katika zahanati ya Makuburi.
Zahanati hiyo ipo katika mtaa wa Mwongozo kata ya Makuburi Manispaa ya Kinondoni.
Akikabidhi hundi hiyo mwishoni mwa wiki kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Bunini Kamba, Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (pichani) alisema hatua hiyo ni muendelezo wa kampuni hiyo, kuchangia huduma za jamii ili kutatua kero zilizopo.
Alisema katika jitihada za kuchangia maendeleo, kampuni hiyo itachimba kisima cha majisafi na kujenga tangi la kuyahifadhi maji hayo, hivyo kuondoa tatizo lililokuwepo hapo awali.
“Huu ni muendelezo wa kampuni yetu kurudisha kidogo faida ya tunachokipata kwa jamii, ambayo imekuwa ikishirikiana nasi vizuri kwa muda mrefu, mbali na eneo hili tayari tumeshatoa misaada kama hii maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam,” alisema Malulu.
Alisema kuwa kampuni imekuwa ikienda kwenye maeneo yenye mkusanyiko wa watu na kutoa misaada ya huduma ya maji, kwa sababu haiwezi kumfuata mtu mmoja mmoja. Alisema wamekuwa wakitoa msaada kwenye maeneo ya mikusanyiko ili huduma iweze kuwa na manufaa kwa watu wengi.
Kwa upande wake, Dk Kamba alisema msaada huo ni muhimu kwa zahanati hiyo na utapunguza gharama zilizokuwa zikitolewa kwa ajili ya kununua maji.
Alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakigharamia huduma za maji katika zahanati hiyo na zinginezo, kwa kuwa miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) haijaifikia zahanati hiyo, hivyo kusogezwa kwa huduma hiyo mahali hapo ni msaada tosha kwao.
“Tumekuwa tukilipia boza la maji kwa kiasi cha zaidi ya Sh milioni 3 kila mwezi kwa ajili ya kusambaza katika zahanati zenye uhaba wa maji ikiwemo zahanati ya makuburi, hatua hii ya leo itatusaidia kupunguza gharama hizo,” alisema Dk Kamba.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Dk Stela Kivugo alisema zahanati hiyo inahudumia zaidi wa wagonjwa 250 kwa siku.
Aliongeza kuwa kwa hali hiyo, suala la maji lilikuwa lina umuhimu wake mahali hapo.
“Tatizo la maji ni kubwa sana katika zahanati yetu, tuna miezi mitatu sasa hatujapata maji na hivyo tunalazimika kununua suala ambalo ni gharama kubwa,” alisema Dk Kivugo.