Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

WAFANYABIASHARA NCHINI WASHAURIWA KUTUMIA '.TZ'

$
0
0
Wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni nchini, wameshauriwa kutumia rajisi ya ‘.tz ‘ kujitangaza na kupunguza wimbi la uhalifu wa mitandao.
Utumiaji wa rajisi hiyo, umeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwani wateja wanaopata huduma kupitia mitandao hiyo, huwa na uhakika na huduma inayotolewa.
Aidha unaelezwa kuwa rajisi hiyo ina uwezo mkubwa wa kupambana na uhalifu unaofanywa katika mitandao, kupitia .tz information centre inyohusika na usajili wa rajisi
Akizungumzia suala hilo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendejea, Mhasibu wa .tz information centre, Peter John, alisema, bado watu wengi hawana uelewa wa umuhimu wa .tz.
“Moja kati ya faida hizo ni kukabiliana na uhalifu ambao kwa sasa umeshika kasi kubwa, endapo utapokea ujumbe kwenye barua pepe yako na ikaonyesha ina rajisi ya .tz uwezekano wa kumpata mtu aliyefanya uhalifu ni mkubwa,” alisema.
Alisema mbali na usalama anaopata mteja mwenye rajisi hiyo, lakini pia gharama zake ziko chini.
“Unajua unapotumia rajisi za kijamii ni rahisi zaidi kuibiwa lakini pia huna pa kwenda kulalamika, lakini ukiwa na rajisi ya .tz ni vigumu sana kwa wewe kuibiwa,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

Trending Articles