Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

UBORA WA BIDHAA ZA TANZANIA WAONGEZEKA MAONESHO SABASABA

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete ametembelea Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Sabasaba kwa na kusema ameridhishwa na ubora wa bidhaa za Tanzania ulivyoongezeka, ikiwa ni pamoja na ufungashaji wa kisasa.
Alisema kwa ubora huo ni dhahiri nchi inapiga hatua kuweza kushindana katika masoko mbalimbali duniani. Alisema ubora wa bidhaa hizo, unaridhisha.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda mbalimbali kwa saa tano, Kikwete alisema maonesho ya mwaka huu ni mazuri na mazingira yameboresha.
“Kinachotakiwa ni kuboresha zaidi ubora wa bidhaa na vifungashio, lakini kwa sasa nchi inaweza kujivunia bidhaa tulizonazo ili kuingia katika soko la ushindani,” alisema Rais Kikwete
Akitembelea mabanda hayo, alianza na Banda la Karume ambalo lina washiriki wengi kutoka nje ya nchi. Alisema ameridhishwa na bidhaa na teknolojia mbalimbali, zilizokuwa katika mabanda hayo.
Pia, Rais alitembelea banda la Jeshi la Magereza na kuangalia kilimo cha mahindi, nyanya, mboga na kupata maelezo kuhusu bidhaa hizo, ikiwa ni pamoja na utunzaji wake.
Katika banda hilo, Rais Kikwete alitoa maelezo juu ya kilimo cha kisasa kwa wananchi ili kuwezesha kulima na kupata mazao bora.
Rais alitumia muda mrefu katika banda la Tanzania na kupata maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini, ambapo alipongeza kwa bidhaa hizo bora na ufungashaji wake.
Akiwa katika banda la Kituo cha Kutoa Matibabu ya Viungo la Ceragem  kwa kutumia umeme cha Master V3, kinachotibu magonjwa mbalimbali ya uti wa mgongo, alipatiwa kitanda maalumu kwa ajili hiyo.
Alipofika katika banda la chuo cha Global, kinachosaidia wanafunzi wa Tanzania kupata vyuo mbalimbali nje ya nchi pamoja na kuwapatia wafadhili, alipatiwa nafasi moja ya chuo na kutakiwa kuteua mwanafunzi mmoja wa kupata mafunzo nje ya nchi.
Rais alitembelea pia mabanda ya  Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles