Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

KIKWETE KUPAMBA JUBILEI YA MIAKA 75 YA KANISA LA TAG

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa  kuwa mgeni  rasmi  katika kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), yatakayofanyika Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Michezo wa Sokoine jijini Mbeya.
Hayo yamethibitishwa na Askofu Mkuu wa  Kanisa  la TAG nchini, Askofu Barnabas Mtokambali katika  hotuba yake iliyosomwa juzi na  Askofu  wa Jimbo  la Rukwa, Askofu Aron Shimwela.
Alisema hayo  katika hafla ya ugawaji  wa  shuka  1,300 zilizotolewa na kanisa  hilo. Hafla hiyo ilifanyika katika Hospitali  ya Mkoa  wa Rukwa mjini hapa.
Akifafanua, alisema tangu  kuanza kwa maadhimisho ya Jubilei  ya miaka 75  ya Kanisa la TAG, kanisa limekuwa  likifanya shughuli mbalimbali,  ikiwemo huduma kwa jamii,  ikiwa ni pamoja na kufanya usafi  katika  maeneo  mbalimbali.
Pia wamekuwa wakitembelea  na  kutoa misaada mbalimbali  katika  magereza, vituo vya kulelea watoto yatima, hospitali, zahanati  na  vituo  vya afya,  ikiwa ni pamoja na  kuchangia  damu katika hospitali mbalimbali.
Askofu Shimwela alisema  kuanzia Julai mosi hadi Julai 4 mwaka  huu, Kanisa la TAG limegawa  vyandarua  katika hospitali  na  vituo  vyote  vya afya vinavyomilikiwa  na Serikali, taasisi za dini na binafsi  katika mikoa ya Mbeya, Rukwa na Njombe.
“Vyandarua takribani 8,550 vimegawiwa  katika hospitali 34  na vituo vya afya 83 katika mikoa ya Rukwa, Mbeya na Njombe …Kanisa la TAG  kama sehemu ya  jamii  linatambua  ukubwa wa  tatizo la ugonjwa wa malaria  hasa  kwa  wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
“Hivyo pamoja na kutoa  huduma  ya kiroho  pia tunaunga  mkono jitihada  za Serikali  katika  kufikia  Malengo  ya Milenia  katika mapambano  dhidi  ya malaria,“ alisema Askofu Shimwela.
Katika ghafla  hiyo  ya makabidhiano, Askofu Shimwela  kwa  niaba ya  Askofu Mkuu  wa TAG, alimkabidhi Kaimu Mganga  Mkuu  wa Mkoa  wa Rukwa, Dk Emmanuel Mtika vyandarua  1,300 vitakavyogawiwa  katika  hospitali tatu  na vituo vya afya  22  mkoani humo na  zahanati zinazolaza wagonjwa.
Kwa upande wake, Mkuu  wa Wilaya  ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka alilishukuru kanisa  hilo kwa msaada huo. Pia,  alimtaka Mganga Mkuu  wa Mkoa  wa Rukwa, kuhakikisha kuwa msaada huo unatumika kwa  malengo  yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles