Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

VIGOGO CHUO CHA UHASIBU KORTINI, YUMO MKUU WA CHUO

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Johannes Monyo na wenzake saba wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakituhumiwa kwa makosa manne tofauti yakiwemo ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh 6,258,448.60.
Profesa Monyo na wenzake walisomewa mashtaka manne tofauti jana mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka Adam Kilongozi aliyekuwa pamoja na Hamidu Singano.
Katika shikata la kwanza, Profesa Monyo na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi chuoni hapo, Jerome Augustino  inadaiwa kuwa Septemba 30, 2011 wakiwa waajiriwa kwa nafasi zao  vibaya  kwa kubadilisha matumizi  ya vifaa vya umemejua (solar) kwa manufaa yao binafsi.
Aidha, katika shitaka la pili wanaohusishwa ni Jerome Agustine,  Chacha Wambura, Mpoki Mwasaga, Papias Njaala, Mathew Melita, Mary Thomas, Elisaria Kisanga na Gerald Malisa  ambao inadaiwa kuwa, kwa pamoja wakiwa wajumbe wa bodi ya manunuzi walitumia nyathifa zao vibaya na kuidhinisha manunuzi ya sola hiyo yenye thamani ya Sh 6,258,448.60 kwa kutumia utaratibu wa kuipa zabuni kampuni ya Helvetic Solar Contractrors .
Katika shitaka la tatu, watuhumiwa Augustino ,Faraji Mnyepe na Honory Mkelemi kwa pamoja inadaiwa kuwa kati ya Novemba 1 na 30 mwaka 2011 katika utekelezaji wa majukumu yao, kila mmoja waliwezesha mchakato wa malipo kwa kampuni ya  sola ya Helvetic Solar Contractors kwa kutoa malipo ya Sh 6, 258,448.60
Na shitaka la nne, Profesa Monyo na Augustine wanadaiwa kuwa mnamo Juai na Novemba 30 /2011 wakiwa waajiriwa chuoni hapo kwa nyadhifa tofauti, walikisababishia hasara chuo hicho cha uhasibu kiasi cha Sh 6,258,448.60.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashitaka Kilongozi, washitakiwa wote walikana mashitaka yao na hakimu wa Mahakama hiyo, Mustapher Siyan alitoa masharti ya dhamana ambayo ni kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali na kusaini bondi ya sh milioni 1.
Hata hivyo washtakiwa hao wote walitimiza masharti ya dhamana, huku hakimu akitoa amri ya kukamatwa kwa washitakiwa wengine watatu ambao ni Mwasaga, Melita na Malisa ambao hawakufika mahakamani hapo.
Aliagiza popote walipo wakamatwe ili kufikia Agosti Mosi wafike mahakamani hapo kusomewa mashitaka yao.
Awali kabla ya kusoma kwa kesi hiyo ndani ya chumba cha mahakama baadhi ya watumishi kutoka chuoni hapo walitaka kuwadhibiti waandishi wa habari ambao ni wapiga picha za video wasifanye kazi zao, lakini wanahabari walishinda kutokana na kuwa na kibali cha kupiga picha mahakamani hapo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles