Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

NYALANDU AHIMIZA MAKAMPUNI KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amezitaka kampuni za kitalii nchini kutangaza utalii na vivutio vyake ndani na nje ya nchi  ili kuwapa wananchi moyo wa kizalendo katika kujali vivutio walivyo navyo.
Aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano mkuu wa asasi ya Wamiliki wa kampuni za kusafirisha watalii (TATO)  uliofanyika mjini hapa.
Aidha alisema kampuni hizo zina mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa zinautangaza utalii  na kuongeza kuwa hii ndio nafasi kubwa waliyokuwa hizo kampuni kubwa za uendeshaji shughuli za kitalii.
Waziri Nyalandu pia  amezitaka kampuni hizo  kuhakikisha zinaongeza kiasi kikubwa cha watalii wanaoingia hapa nchini ili kuingizia serikali fedha nyingi za kigeni na kuachana na kasumba iliyozoeleka kupandisha ada ya kiingilio cha kuingia  katika hifadhi pamoja na vivutio kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa TATO, Willey Chambulo ametoa malalamiko yake kwa serikali na kuwakilisha kwa Waziri Nyalandu kuhusiana na tatizo la hivi karibuni kwa kuwepo kwa mageti yasiyo rasmi katika baadhi ya hifadhi hapa nchini.
Alisema kuwa hii imetokea  hivi karibuni katika mbuga inayomilikiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Julai mosi mwaka huu  na kudaiwa ongezeko la kodi pasipokuwa na taarifa na hivyo kuwapa usumbufu kufanya kukamatwa kwa watalii waliokuwepo kuzuiliwa na kuwekwa chini ya ulinzi hivyo kurudisha nyuma hali ya utalii hapa nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles