Serikali imeingia mkataba na Kenya wa kuuza mahindi tani 200,000. Shughuli hiyo itaanza ndani ya wiki mbili zijazo.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
Chiza alikuwa akizungumzia ziara yake ya siku mbili nchini Kenya, aliyokwenda kwa mwaliko wa Waziri wa Kilimo na Chakula wa nchi hiyo.
Chiza alisema Tanzania imekubali kuiuzia Kenya tani hizo 200,000 za mahindi ambazo zitauzwa kwa awamu na kwamba awamu ya kwanza itakuwa ni tani 50,000 za mahindi kutoka hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).
Aidha tani 150,000 zinazobaki zitanunuliwa kutoka kwa wakulima ambapo wafanyabiashara wenye vibali, watasimamiwa na NFRA, kwenye ununuzi wa mazao hayo kutoka kwa wakulima, ili kuhakikisha ubora wa mahindi unazingatiwa na pia bei inayotolewa ni stahiki kulingana na gharama za uzalishaji wa mkulima.
Alisema makubaliano hayo yanafanyika wakati Kenya wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, ambao umesababisha wafanyabiashara nchini humo kuficha mahindi na kuwalangua walaji.
Aliongeza katika ziara hiyo ya siku mbili, ambayo alirudi nchini juzi, aliongozana na baadhi ya wafanyabiashara ambao baada ya kukubaliana na waziri wa Kenya kuwauzia mahindi, wafanyabiashara hao wa Tanzania ndio watakuwa na jukumu la kununua mahindi hayo na kwenda kuyauza Kenya.
Alisema, kukubali kuwauzia Kenya mahindi kunatokana pia na uwepo wa chakula cha kutosha nchini, ambapo hivi sasa NFRA, ina utoshelevu wa chakula zaidi ya asilimia 118, ambacho ni mavuno ya msimu uliopita.
Alisema leo makatibu wakuu wa wizara hizo mbili za Kenya na Tanzania wanakutana jijini Arusha kwa ajili ya kusaini mkataba wa makubaliano kuhusu uuzaji wa mahindi hayo(MoU), ili utekelezaji wake uanze mapema ndani ya wiki mbili zijazo.